24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

ARNOLD SCHWARZENEGGER ACHOKA KUKAA NDANI

LOS ANGELES, MAREKANI



STAA wa filamu nchini Marekani, Arnold Schwarzenegger, ameweka wazi kuwa, amechoka kukaa ndani kama mfungwa, tangu alipofanyiwa upasuaji wa moyo.

Schwarzenegger, mwenye umri wa miaka 70, alikuwa anasumbuliwa na tatizo la moyo na baada ya kufanyiwa upasuaji Machi 29, amekuwa mtu wa kukaa ndani, lakini sasa amedai kuwa, amechoka na ameamua kutembea mitaani kukutana na mashabiki zake.

“Nina furaha kuona nipo kwenye afya nzuri, mimi si mfungwa ambaye ninaweza kukaa ndani kwa kipindi kirefu, hivyo kutokana na hali yangu kuwa sawa nimeona bora nitembee mitaani kukutana na mashabiki.

“Najua mashabiki walikuwa wanatamani kukutana na mimi, hivyo nataka kuwaambia kuwa nipo sawa na nina furahi kuwaona na ninashukuru kwa salamu zao za pole,” alisema Schwarzenegger.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles