ARIANA GRANDE AWAFARIJI WATOTO HOSPITALI

0
529

MANCHESTER, ENGLAND


NYOTA wa muziki nchini Marekani, Ariana Grande, jana aliwatembelea baadhi ya majeruhi waliolipukiwa na bomu jijini Manchester dakika chache baada ya kumalizika kwa shoo yake.

Uamuzi huo unakuja baada ya wiki moja kupita msanii huyo alipofanya shoo jijini Manchester kwenye ukumbi wa Manchester Arena, wenye uwezo wa kuchukua watu 21,000 na kutokea mlipuko wa bomu ulioua watu 22 na majeruhi 119.

Msanii huyo alianza kutembelea katika Hospitali ya ‘Royal Manchester Children hospital’ ambapo kulikuwa na baadhi ya watoto waliolazwa kutokana na kuathirika na mlipuko huo.

“Kabla ya kuanza kwa shoo yangu leo (jana), nimeanza kwa kuwatembelea baadhi ya watoto waliojeruhiwa na mlipuko wa bomu, furaha yangu ni kuwaona wakiendelea vizuri,” alisema Ariana.

Hata hivyo, usiku wa jana msanii huyo alikuwa na ratiba ya kufanya shoo ya kuwafuta machozi ndugu na jamaa waliopoteza ndugu zao, huku mastaa kibao akiwamo Justin Beiber, Pharrell Williams na wengine wengi wakiungana naye kutumbuiza katika shoo hiyo iliyopewa jina la ‘All Star Benefit Concert’.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here