24.8 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

Apple Music yasherehekea shamrashamra za umoja kwa ajili ya mwezi wa Afrika

Na Mwandishi Wetu

Wakati macho na masikio ya dunia kwa sasa yakiwa yameelekezwa Afrika, Apple Music inasherehekea Mwezi wa Afrika, Mei hii kwa kampeni yenye kauli mbiu ya ‘umoja na ujumbe wa mshikamano’.

Kampeni hii pia inamulika kizazi kipya cha wasanii wa Afrika wanaobadilisha simulizi katika tasnia ya muziki nyumbani na ng’ambo.

Kampeni inahusisha playlist mahususi ya umoja kwa ajili ya Mwezi wa Afrika inayojumuisha baadhi ya nyimbo bora za kushirikiana barani za hivi karibuni, kukiwa na muziki kutoka kwa Focalistic na Davido, Naira Marley na Busiswa, Gyakie akimshirikisha Omah Lay pamoja na AKA akimshirikisha Burna Boy.

Pia pamejumuishwa playlist 12 ngeni na mahususi kutoka kwa wasanii wakiwemo Omah Lay (Nigeria), Manu Worldstar (Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo/Afrika Kusini), Tems (Nigeria) na Amaarae (Ghana), wote wakiwa wamewahi kuhusishwa kwenye mpango wa Apple Music wa kuwangaaza wasanii wanaochipukia, Africa Rising.

Wakiwakilisha nchi za Afrika zinazozungumza Kireno (Lusophone) wapo Nenny (Cape Verde) na Calema (São Tomé and Príncipe), kutoka Afrika Mashariki ni Zuchu (Tanzania) na Nviiri The Storyteller (Kenya), kwa nchi za Afrika zinazozungumza Kifaransa (Francophone) tunaye Suspect 95 (Ivory Coast) na Tayc (Cameroon), na mwisho wakiwakilisha nchini za Kusini mwa Afrika, tunaye Focalistic (Afrika Kusini) na mshindi wa tuzo ya BET Sha Sha (Zimbabwe).

Orodha hizi za kucheza zimeundwa na nyimbo zinazowafanya wasanii wajivunie kuwa Waafrika au ambazo zimebadilisha sura ya muziki wa Afrika.

Mwezi wa Afrika utaungwa mkono pia kupitia Apple Music Radio, Africa Now Radio na Cuppy kitaendesha kipindi kwa ajili ya Mwezi wa Afrika maalum kwa ‘Umoja’ Jumapili ya Mei 30 kusherehekea kutimiza mwaka mmoja ya kipindi hicho na kutoa heshima kwa baadhi ya nyimbo bora za ushirikiano barani.

Kwenye The Ebro Show cha Apple Music 1, kila wiki Ebro atamhoji mgeni kutoka kanda tofauti kuzungumza kuhusiana na playlist yao maalum ya Mwezi wa Afrika pamoja na kuhusisha mchanganyiko wa muziki wenye hamasa (Motivation Mix) kila wiki kutoka kwa Madj maarufu barani Afrika wakicheza nyimbo bora za Amapiano, Afrobeats na zingine.

Nadeska pia atamhusisha msanii anayechipukia wa wiki kwenye kipengele chake cha Africa Rising kila wiki katika mwezi Mei.

Wasanii waliohusishwa walikuwa na haya ya kusema kuhusiana na playlist hizi:

“Nilichagua nyimbo hizi kwasababu zinawakilisha ukuaji wa Afrobeats katika miaka hii, kuonesha jinsi ladha za mahadhi haya zilivyo za aina mbalimbali. Nilipangilia playlist hii kuonesha mchanganyiko huo katika sauti na kila wimbo una mkasa wake wenyewe wa mchango wake kwenye Afrobeats,” Omah Lay ameiambia Apple Music.

“Nyimbo hizo zinanisafirisha katika nyakati tofauti kwenye maisha yangu na kunikumbusha jinsi muziki unavyoweza kukurudisha nyuma mahala fulani na hisia.” – Tems

“Ninachokipenda zaidi kuhusu nyimbo hizi ni maana zake Kiuafrika. Kuna mdundo na nguvu kuhusu Afrika ambayo inaelezewa vyema zaidi kupitia muziki wetu. Ningependa kila mmoja kuzielewa nyimbo hizi zinazoakisi nguvu yetu na uzuri kama Waafrika. Mwezi wa Afrika unawakilisha kile ninachosimamia na kusikiliza kila siku nikiwa nimepumzika, nikifurahia au kujiachia. Hakika napenda kusambaza playlist yangu kwa yeyote na mwezi wa Afrika ni wakati bora kufanya hivyo kwasababu muziki wa Afrika unazungumza nami. Ninatumaini hiki kitazungumza nawe pia.” – Sha Sha

“Hizi nyimbo zinanifanya nijisikie fahari kuwa Mwaafrika. Wabunifu wenye akili nyingi na halisi kutoka kwa wasanii hawa wa Afrika kunanifanya nijivunie na hakika Afrika kwa ulimwengu ni mkakati muhimu. Nina hamu kuona Sghubu ya Afrika ikiteka dunia na kwa utamaduni kuenea kwenye vizazi zaidi! SGHUBU SES EXCELLENT KUTOKA KWANGU KWENDA KWAKO!” – Focalistic

“Nyimbo za jana zilizotuzaa tulivyo leo. Mkusanyiko huu wa nyimbo unapitia mirindimo iliyopewa nguvu kisiasa, mapigo ya zamani na mashairi ya miaka 70, mafumbo mepesi ya kimapenzi na utayarishaji mseto wa R&B/Hiphop ya magharibi ya kati hadi highlife ya mwishoni mwa 90 pamoja na hip life na kisha mlipuko wa Afrobeats ya miaka ya 2010 iliyotengeneza njia mpya ya muziki wa Afrika. Nyimbo hizi ni sababu mimi ni mimi na wewe ni wewe. Tumeishi nazo katika maisha yetu yote kupitia wazazi wetu, marafiki na wapenzi wetu. Leo hii tunasherehekea wasanii waliosababisha nyakati hizi ziwezekane.” – Amaarae

“Tunapata mahadhi mbalimbali ya muziki wa asili yangu ya Cape Verde kama vile Funana na Morna. Na pia ladha zingine za Kiafrika kama Souk na Gqom ambazo zimekuwa zikinipa kampani. Ninaposikiliza playlist hii nisingechagua chochote lakini kuwa Mwafrika.” – Nenny

“Muziki umekuwa sauti ya muda wote kwetu sote – kutuunganisha, kutunyanyua na kuburudisha vizazi vyote. Umekuwa chombo kisicho na mwisho kilichotumika kuzungumza hadithi zetu zisizosimuliwa,” anasema Nviiri The Storyteller

“Hizi ni nyimbo zangu pendwa za muda wote kwakuwa zinanihamasisha kuandika nyimbo zitakazoishi vizazi vyote,” anasema Zuchu.

“Playlist hii ndicho ninachokitafsiri kama Afrika Mpya. Afrika iliyochangamka. Nyimbo hizi hazijanihamasisha tu lakini pia zimenijenga kuwa msanii niliye leo,” Manu Worldstar.

Kwa muda ulio na kikomo, wateja wapya wa Apple Music kwenye iOS na Android katika nchi za Nigeria, Afrika Kusini, Ghana, Kenya, Botswana, Tanzania, Uganda, Msumbiji, Cameroon na Zambia wanaweza kufurahia maudhui yote bora bure kwa miezi 6 kwenye Apple Music kupitia app ya Shazam. Wateja wanaorejea wanapata miezi 3 bure katika Apple Music.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,264FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles