‘App’ inayobana trafiki wala rushwa yazinduliwa

0
910

LEONARD MANG’OHA-DAR ES SALAAM

SERIKALI imezindua mfumo mpya wa kielektroniki unaofahamika kama ‘Takukuru App’ utakaotumika kudhibiti askari wa usalama barabarari wanaojihusisha na vitendo vya rushwa.

Uzinduzi wa mfumo huo umefanyika sambamba na uzinduzi wa kampeni ya Utatu inayolenga kuongeza mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa barabarani kwa kushirikisha Takukuru, Jeshi la Polisi na wadau mbalimbali.

Mfumo huo wa ‘Takukuru App’ utawezesha wananchi kutuma taarifa za vitendo vya rushwa vinavyofanyika sehemu mbalimbali nchini kwenda Takukuru.

Kupitia mfumo huo mwananchi anaweza kuupakuwa na kuwa nao kwenye simu yake ya mkononi  utamwezesha kuonesha eneo ambapo tukio  la rushwa linafanyika, kutoa ufafanuzi wa tukio lenyewe ili maofisa wa Takukuru waweze kufuatilia, kisha atatuma ujumbe huo kwenda Takukuru na kupewa mrejesho wa kupokewa kwa ujumbe alioutuma.

Pia mfumo huo utaliwezesha Jeshi la Polisi kuona taarifa hizo na kufanya uchunguzi kisha kutoa mrejesho wa hatua zilizochukuliwa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika, aliwataka wananchi kutoa taarifa za kweli kupitia App hiyo bila kuwaonea watu waliokosana nao kwa mambo binafsi.

Mkuchika alisema kuwa mfumo huo utarahisisha mapambano dhidi ya rushwa kuanzia kwa wananchi wenyewe hadi Takukuru.

Kuhusu kampeni ya Utatu aliwataka wananchi kuwa sehemu ya mapambano dhidi ya rushwa barabarani ambayo imekuwa chanzo cha madhara mbalimbali ikiwamo ajali za barabarani.

Pia Mkuchika alisema tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa nchi za Bara la Afrika hupoteza kati ya asilimia moja hadi tatu ya mapato yake kugharamia madhara yatokanayo na ajali za barabarani.

Mkuchika alisema kampeni ya Utatu haiwezi kufanikiwa endapo kazi ya kupambana na rushwa wataachiwa Takukuru pekee pamoja na mamlaka nyingine za Serikali.

Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro, alisema matumzi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) yatasaidia kupunguza vitendo vya rushwa barabarani kwa sababu vitapunguza nafasi ya askari wa usalama barabarani na wasimamizi wengine wa sheria kukutana na watu wanaovunja sheria.

Sirro alisema kutokana na hatua mbalimbali zinazochukuliwa kudhibidhi vitendo vya rushwa na ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani umesaidia kupunguza ajali kwa asilimia 57.

“Baada ya uzinduzi huu wa Utatu kinachofuata ni vitendo, ndivyo vitapunguza rushwa, uzinduzi huu utakuwa na maana wadau wote wakishiriki,” alisema IGP Sirro.

Mkurugenzi wa Uzuiaji Rushwa wa Takukuru, Sabrina Seja, alisema kampeni ya Utatu imeanzishwa kwa lengo la kuzuia rushwa barabarani ambayo imekuwa chanzo kikuu cha ajali.

Alisema ajali zyingi zimekuwa zikishababishwa na baadhi ya askari wa usalama barabarani kujihusisha na rushwa, mioundombinu mibuvo na uzembe.

“Lakini pia madereva wengi hawana mikataba hali anyowapa mawazo, rushwa pia hutumika kupata mafunzo na leseni. Kwa hiyo kampeni hii itatufanya tutafakari kwa pamoja hatuia za kuchukua,” alisema Sabrina.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here