Apata corona akiwa gerezani

0
1379

 TEHRAN, IRAN

FATEMEH Khishvand, mashuhuri kwa jina la Sahar Tabar katika mtandao wa Instagram, baada ya kutuma picha zake mtandaoni ambazo zimeelezwa na wengi kama ‘zombie’ wa Angelina Jolie, amesema amembukizwa ugonjwa wa corona akiwa gerezeni.

Khishvand alikamatwa mwishoni mwa mwaka jana kwa makosa ya uhalifu, ikiwamo kukufuru na kuchochea ghasia.

Lakini mkuu wa gereza ambapo anazuiliwa, amekanusha madai ya ameambukizwa virusi hivyo.

“Kuna taarifa zilizotolewa na wakili Fatemeh Khishvand ambazo si za kweli na ninazikanusha,” Mehdi Mohammadi, mkuu wa gereza la wanawake la Shahr-e Rey, ameliambia Shirika la Habari la ISNA la Iran.

Iran imekuwa na idadi kubwa ya vifo kwa sababu ya virusi vya corona mashariki ya kati, huku idadi mpya zilizotangazwa na Msemaji wa Wizara ya Afya, ikifia zaidi ya 5,000.

Hatahivyo, kuna wasiwasi idadi halisi ya waliokufa ikawa juu zaidi ya hiyo.

Wakili wa Khishvand, Payam Derafshan aliandika barua ya wazi kwa mahakama ya Iran ambayo aliituma kwenye akaunti yake ya Instagram.

Alisema amearifiwa na mama yake Khishvand kuwa mteja wake, amehamishwa hadi eneo la karantini ndani ya gereza baada ya kuonesha dalili za virusi vya corona.

 Alisema Khishvand ambaye alikuwa na umri mdogo, wakati anashtumiwa hatafanikiwa kutoka na kufuatilia kesi yake akiwa nje kwasababu bado inaendelea.

Machi, mwaka huu, Iran iliwaachia huru wafungwa 85,000, akiwemo mhudumu wa shirika la kutoa msaada raia wa Uingereza mzaliwa wa Iran – kama sehemu moja ya kukabiliana na virusi hivyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here