30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Apandishwa kizimbani kwa ubakaji

GODFREY SHAURI – DAR ES SALAAM

MKAZI wa Tegeta Machinjioni, Shadrack Shaibu (24), amepandishwa kizimbani Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kujibu shtaka linalomkabili la ubakaji.

Awali akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi John Chacha, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Dorth Massawe  alidai mnamo Desemba 26 mwaka 2018 maeneo ya Tegeta Machinjioni mshtakiwa alimbaka binti mwenye umri wa miaka 16 ambaye jina lake limehifadhiwa.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo na Massawe alisema upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kuomba tarehe kwa ajili ya kusomwa tena kwa shauri hilo.

Hakimu Chacha alisema kesi hiyo ina dhamana endapo mtuhumiwa atakidhi masharti ya kuwa na wadhamini wawili waaminifu watakaotoa kiasi cha Sh 500,000 kwa kila mmoja na wenye barua kutoka kwenye taasisi zinazotambulika au barua kutoka Serikali za mitaa.

Hata hivyo mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana, hivyo alirudishwa rumande hadi Machi 25 atakaporudi tena mahakamani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles