22.5 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

ANYWA MAJI YA BETRI KWA WIVU WA MAPENZI

Na Ibrahim Yassin-Njombe


 

maji-ya-betriMKAZI wa Kijiji cha Kimelembe wilayani Ludewa, mkoani Njombe, Maria Kayombo (31) amenusurika kifo baada ya kunywa maji ya betri kutokana na wivu wa kimapenzi.

Akizungumza na MTANZANIA jana, mama mzazi wa mwanamke huyo Magdalena Kayombo alisema tukio hilo lilitokea juzi ambapo alipigiwa simu akiwa shambani kuwa hali ya mtoto wake ni mbaya baada ya kunywa sumu.

Alisema walimkimbiza katika zahanati ya jirani ambapo alipatiwa matibabu na kumweleza kuwa alikuwa amekunywa maji ya betri baada ya kugombana na mumewe, Peter Henjewele akimtuhumua kuwa na ‘mchepuko’.

“Sikuweza kumhoji sana kwani nilishikwa na mshangao aliponiambia amekunywa maji ya betri ili afe amuache mumewe aendelee kuwa na mchepuko,” alisema.

Akizungumzia hali hiyo baada ya kupata nafuu mwanamke huyo alisema chanzo cha yeye kuchukua uamuzi huo ni kitendo cha mume wake kuwa na wanawake wengine nje.

“Tulianza nae maisha katika hali ngumu, kitendo cha kuanza kuchepuka wazi wazi na wanawake wengine ni dharau nikaona bora nife kuliko kuvumilia maumivu hayo ya kimapenzi,” alisema.

Hata hivyo, mume wa mwanamke huyo, alitokomea kusikojulikana baada ya kuona mke wake amekunywa maji ya betri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles