27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

Anyang’anya askari magereza SMG, auawa na polisi

Elizabeth Kilindi, Njombe

KIJANA mmoja aliyefahamika kwa jina la Isaack Kawogo (24) aliyempora askari magereza bunduki aina ya SMG mkoani Iringa, ameuawa kwa kupigwa risasi na polisi baada ya kumjeruhi kaka yake Andres Kawogo (61) akimtuhumu kuuza mashamba na kushindwa kumtoa gerezani.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Hamis Issah, alisema tukio hilo limetokea Novemba 20 saa 10:45 alfajiri huko maeneo ya Chaugingi mjini Njombe.

Alisema kijana huyo aliiba silaha na kuitumia kufanya uhalifu ambapo alifanya matukio kadhaa mkoani Iringa ikiwemo kumshambulia askari kwa panga hali iliyosababisha wafungwa wengine kutoroka.

“Hii ni silaha ambayo askari magereza wanaitumia katika ulinzi wa wafungwa hao, sasa huyu kwakuwa ni mhalifu akawa anaitumia katika uhalifu,”alisema Issah.

Alisema silaha hiyo ilikuwa na risasi 10 lakini hadi inakamatwa na askari ilikuwa imebakiwa na risasi mbili pekee huku nane zikiwa zimetumika kufanya uhalifu maeneo tofauti ikiwemo tukio lilotokea mkoani Njombe la kumjeruhi kaka yake.

Alisema juhudi za kutaka kuokoa maisha ili alieleze alivyoondoka na silaha hiyo hazikifanikiwa.

Aliwataka wahalifu wenye tabia ya kuwashambulia askari na kuwanyang’anya vitendea kazi kuacha tabia hiyo kwani jeshi hilo halitakuwa tayari kufumbia macho matukio kama hayo.

“Ukimnyang’a askari silaha namna pekee ya kuipa hiyo silaha ni kwa kutumia silaha, hivyo wanapaswa kuwa makini”alisema Issah.

Pia Kamanda Issah aliwataka wananchi kuwa na tahadhari na wahalifu sugu pindi wanapotoka magerezani na kuacha tabia ya kuwaficha kwani kufanya hivyo kunatajwa kukithiri matukio ya kihalifu mkoani Njombe licha ya jeshi hilo kuthibiti matukio hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles