26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Angola yaahidi kumrejesha Isabel Dos Santos

Luanda, Angola

WAENDESHA mashtaka nchini Angola wamesema kuwa watatumia njia zote zinazowezekana kufanikisha zoezi la kurejeshwa nchini mfanyabiashara na binti wa rais wa zamani wa nchi hiyo, Jose Eduardo dos Santos.

Maofisa hao wamesema kuwa watatumia njia zote zinazowezekana kumrejesha nchini Isabel dos Santos, binti bilionea baada ya maelfu ya nyaraka zilizovuja kuonyesha madai mapya kwamba alichota mamia ya mamilioni ya fedha za Serikali ya nchi hiyo.

Binti huyo aliyepewa jina la “mwanamke tajiri zaidi barani Afrika”, anatuhumiwa kutumia nafasi ya baba yake kuiba fedha za Serikali katika nchi hiyo tajiri kwa mafuta lakini iliyosalia masikini.

Isabel anatuhumiwa kuiba fedha hizo za umma kwa kusaidiwa na kampuni za ushauri za nchi za Magharibi na kuzihamishia nje ya nchi.

Alihama Angola baada ya baba yake, aliyetawala nchi hiyo kwa karibu miaka 40, kuondoka madarakani mwaka 2017 na nafasi yake kuchukuliwa na Joao Lourenco.

Isabel aliye na umri wa miaka 46 ambaye hutumia wakati wake mwingi kati ya London na Dubai, amekanusha tuhuma hizo akisema hazina msingi wowote.

Akizungumza kupitia redio ya umma wiki hii, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Angola, Helder Pitra Gros alisema kuwa watatumia njia zote zinazowezekana na kuomba msaada wa kimataifa ili kumrejesha nchini Isabel.

Alisema tayari wameomba msaada wa kimataifa kutoka Ureno, Dubai na nchi nyingine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles