27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

ANGELINA: PITT ATABAKI KUWA MUME WANGU

NEW YORK, MAREKANI


MKALI wa filamu nchini Marekani, Angelina Jolie, amefunguka kwa mara ya kwanza tangu kusambaa kwa taarifa za kuachana na Brad Pitt, amedai kuwa ataendelea kuwa mume wake daima.

Mrembo huyo amesema kuwa, alikuwa katika wakati mgumu kuelezea kilichotokea kati yake ya mume wake, lakini kwa sasa kila kitu kipo sawa.

“Nilikuwa nashindwa kuelezea kilichotokea, lakini kwa sasa naweza kusema kuwa kila kitu kipo sawa, Brad Pitt ataendelea kuwa baba wa familia yangu.

“Najua hali niliyoipitia mimi watu wengi wamepitia, najua sikuguswa peke yangu, kitu ambacho kilikuwa kinaniumiza ni watoto wangu, lakini nina furaha kubwa kumaliza tofauti zetu,” alisema Angelina. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles