23.9 C
Dar es Salaam
Friday, September 30, 2022

ANGELINA JOLIE AMUUMBUA BRAD PITT

LONDON, ENGLAND


STAA wa filamu nchini Marekani, Angelina Jolie, amemuumbua aliyekuwa mume wake, Brad Pitt, kwa madai kuwa bado hana msaada kwa familia yake ya watoto sita.

Miezi kadhaa iliyopita, kulikuwa na taarifa kwamba Pitt amempa mrembo huyo kiasi cha dola milioni 9 kwa ajili ya huduma za watoto wake, lakini mrembo huyo amedai fedha hizo amemkopesha na si kumpa kwa ajili ya watoto wake kama ilivyoripotiwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

Angelina amedai tangu waachane Septemba 2016, baba huyo wa watoto wake hana msaada wowote na fedha hizo alizokopa kwa ajili ya kununua nyumba pamoja na kulipa kodi ya nyumba aliyokuwa anakaa na watoto wake.
Mwanasheria wa mrembo huyo anatarajia kufika mahakamani kwa ajili ya kumlalamikia Pitt kwa kushindwa kuhudumia familia yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,298FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles