27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

ANDY MURRAY ATOLEWA INDIAN WELLS

CALIFORNIA, MAREKANI


BINGWA namba moja kwa ubora wa tenisi duniani kwa upande wa wanaume, Andy Murray, ameyaaga mashindano ya Indian Wells baada ya kuchezea kichapo kutoka kwa mpinzani wake, Vasek Pospisil kutoka Canada.

Murray alionekana kuzidiwa katika mchezo huo juzi dhidi ya bingwa namba mbili kwa ubora nchini Canada, wakati akishika nafasi ya 129 kwa ubora duniani lakini mchezo wa juzi alifanikiwa kushinda kwa seti 6-4 7-6 (7/5).

“Sijui kwanini nimepoteza mchezo huo, kwa sababu katika maandalizi nilikuwa nafanya vizuri, lakini hali hii kuna miaka inatokea na kuna wakati inakuwa ngumu, ila nitahakikisha nafanya mazoezi ya nguvu kurudisha heshima yangu.

“Nashangaa kuona sijaonesha kiwango changu mbele ya mashabiki wangu, lakini nampongeza mpinzani wangu kwa kuonesha kiwango kizuri na kuweza kusonga mbele hatua inayofuata, amestahili kushinda na nadhani alikuwa na mazoezi ya nguvu,” alisema Murray.

Kwa upande mwingine, mpinzani wake Murray, Pospisil, amedai ni jambo la furaha kwake kuweza kushindana na mchezaji bora duniani na kushinda kwenye michuano hiyo mikubwa.

“Hakuna ambaye anajua jinsi ninavyojisikia baada ya ushindi huu, ukweli ni kwamba yametokea, ilikuwa kama ndoto lakini ndivyo ilivyo, halikuwa jambo rahisi kushinda dhidi ya Murray.

“Ushindi huu umenifanya kuwa na nguvu zaidi na kujiamini kwamba naweza kupambana na mpinzani yeyote na nikashinda, hivyo kikubwa ni kuhakikisha nafanya maandalizi makubwa ili niweze kupambana na wapinzani mbalimbali nitakaokutana.

“Ninaamini nikiendelea kufanya mazoezi ya nguvu nitakuwa tayari kupambana na mchezaji yeyote, ninajiamini kutokana na uwezo wangu, kumshinda bingwa namba moja ni jambo la historia kubwa katika maisha yangu ya tenisi,” alisema Pospisil.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles