24.8 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

‘ANDIKA CHALLENGE’ KUCHEMSHA BONGO WANAFUNZI KINONDONI, UBUNGO

Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Taasisi ya Dk. Ntuyabaliwe imeanzisha mashindano ya utunzi wa hadithi nchi nzima liitwalo ‘ANDIKA CHALLENGE’ katika Wilaya za Kinondoni na Ubungo.

Mashindano hayo yamezinduliwa leo Mei 13, jijini Dar es Salaam, katika Shule ya Msingi Kinondoni huku walengwa wakiwa ni wanafunzi wa darasa la nne la na saba ambapo washindi watano watapatiwa zawadi ikiwamo za Kufunguliwa akaunti benki.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Jacqueline Mengi, amesema shindano hilo litadumu kwa mwezi mmoja, baada ya hapo litahamia wilaya nyingine.

Amesema zawadi nyingine watakazopata washindi ni kununuliwa madaftari, sare za shule na vitabu vya mwaka nzima, begi la shule, kombe kwa shule bora na hadithi za watoto watano bora zitatengenezewa kitabu.

“Watakaoshiriki shindano hili watatakiwa kuandika hadithi zenye ubunifu na kwa kutumia akili zao na iwe na mafunzo.

“Tumeanzisha shindano hili kwa sababu tunaamini watoto watajifunza jinsi ya kujieleza maandishi na itaibua vipaji vya watoto kwa kuwa wataweza kuandika hadithi ambazo zitawafunza wengine.

Jacqueline amesema ni matarajio yao wazazi watawahamasisha watoto wao kuingia kwenye shindano hilo na wanafunzi wanaweza kuandika hadithi na kuambatanisha na michoro.

“Lengo la taasisi yetu kukarabati maktaba na kuweka vitabu vya hadithi na Shule ya Msingi Kinondoni ilikuwa ya kwanza kuitembelea baada ya kuzinduliwa kwa taasisi yetu.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Kaimu Ofisa wa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Ester Kahaya ambaye alipongeza taasisi hiyo na kusema serikali inatambua mchango wake katika kukuza sekta ya elimu ambapo ametoa wito kwa wanafunzi kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye shindano hilo kwa kuwa hadithi watakazotunga zitasaidia kukuza lugha ya Kiswahili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,268FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles