25.2 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

Ancelotti ataendeleza ubabe dhidi ya Klopp leo?

LIVERPOOL, ENGLAND

KOCHA wa Everton, Carlo Ancelotti atakiongoza kikosi chake kuwakabili wapinzani wao wa jiji moja, Liverpool katika mchezo wa Kombe la FA utakaochezwa kwenye Uwanja wa Anfield, Liverpool.

Kitu ambacho kinasubiriwa kwa hamu ni kuona kama kocha huyo ambaye amekabidhiwa mikoba ya kuinoa Everton hivi karibuni ataendeleza ubabe wake dhidi ya majogoo hao wa jiji.

Ancelotti ndiye kocha pekee aliyeifunga Liverpool tangu kuanza msimu huu,kocha huyo wa zamani wa Napoli aliikutana na Liverpool katika michezo miwili ya hatua ya makundi ya Ligi Mabingwa Ulaya.

Mkufunzi huyo wa kimataifa wa Italia, aliiongoza Napoli kuvuna pointi nne ktaika michezo hiyo miwili dhidi ya Mabingwa hao wa Ulaya, akishinda mechi moja na kutoka sare moja.

Rekodi za jumla zinaonyesha kuwa, Ancelotti amekumbana na kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp mara sita katika michuano ya Ligi ya Mabingwa na kushinda mechi tatu, akipoteza mbili na kutoka sare moja.

Liverpool imecheza mechi nne za Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Napoli iliyokuwa chini ya Ancelotti katika kipindi cha misimu miwili, ikishinda michezo miwili nyumbani, huku Napoli ikishinda miwili nyumbani na mmoja ugenini.

Mara ya mwisho Ancelotti kutua Anfield aliambulia sare ya bao 1-1 katika mchezo wa marudiano Ligi ya Mabingwa uliochezwa Novemba 27, mwaka jana.

Ancelotti ambaye amepokea kijiti hicho kutoka kwa Marco Silva, atakuwa akiiongoza Everton katika mchezo wake wa pili tangu akabidhiwe mikoba ya kuinoa timu hiyo, akianza kuchapwa na Manchester City mabao 2-1 katika Ligi Kuu England.

Liverpool itaingia katika mchezo huo bila ya huduma ya kiungo wake, Naby Keita ambaye aliumia dakika za mwisho kabla ya mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Sheffied United.

Ancelotti anatekuwa akiiongoza Everton kusaka ushindi wake wa kwanza dhidi ya Liverpool tangu mwaka 1999.

Real Madrid, Juventus zashindana kwa ofa kumng’oa Pogba

MADRID,HISPANIA

KLABU za Real Madrid na Juventus kila mmoja imewasilisha ofa yake kwa ajili ya kuinasa saini ya kiungo wa Manchester United, Paul Pogba, ambaye ameonyesha nia kutaka kuondoka Old Trafford.

Madrid imemuweka chambo kiungo wao, Toni Kroos ili kuishawishia United kumruhusu kiungo huyo raia wa Ufaransa kujiunga na mabingwa hao wa zamani wa Ulaya.

Kwa muda mrefu kocha wa Madrid, Zinedine Zidane ameshindwa kuficha hisia zake za kutaka kufanya kazi na Pogba.

Madrid ilijaribu kuinasa saini ya Pogba katika dirisha kubwa la usajli mwezi Juni mwaka jana, lakini jaribio hilo lilikwama mwishoni licha ya vigogo hao wa Hispania kuwa tayari kuwatoa wachezaji wake, Gareth Bale na James Rodriguez kwenda United.

Wakati, Madrid ikiwa tayari kumuachia kingo wao huyo wa Ujerumani, JJuventus nayo imebisha hodi Old Trafford na kuweka mezani ofa ya kiungo wao, Adrien Rabiot pamoja na kitita cha Euro milioni 60 kwenda Manchester United ili kuishawishi kumuachia Pogba.

Juve inataka kumrudisha tena kiungo huyo waliyoomuuza kwa dau la Pauni milioni 89 miaka minne iliyopita.

United inakabiliwa na wakati mgumu wa kumshawishi Pogba kubaki ndani ya timu hiyo kutokana na ofa hizo zilizowasilishwa kutoka klabu hizo.

Pogba mwenyewe ameonyesha dalili za kutaka kutimka ndani ya timu hiyo kutokana mwenendo mbovu wa matokeo kwa misimu miwili sasana kusshindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita.

Wakala wa mchezaji huo, Mino Raiola alikuwa akishinikiza United imuachie mteja wake kujiunga na moja ya timu hizo zilizoonyesha nia ya kufanya nae kazi katika dirisha la usajili lililopita bila mafanikio.

Hata hivyo, United ilikuwa ikitaja dau kubwa au kutamka haiko tayari kumuuza, hali iliyotibua uhusiano baina na wakala huyo na mabosi wa klabu hiyo.

Baada ya kukwama kwa mpango huo, Raiola aliamua kuikomesha United kwa kumpeleka mteja wake mwingine, Erling Halaand kujiunga na Borussia Dortmud,licha ya United kumuhitaji kwa udi na uvumba.

Hivi karibuni, Raiola alikaririwa akisema hatapeleka tena mteja wake ndani ya klabu hiyo kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa uendashaji wa timu hiyo iliyopteza mvuto wake.

- Advertisement -
Previous articleBAHATI YAO
Next articleJafo awashukia maofisa utumishi

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,784FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles