22.5 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Anayetuhumiwa kumuua, kumchoma mkewe aomba apewe simu amlipie mwanawe ada

Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Mshtakiwa Hamisi Luwongo anayetuhumiwa kumuua mkewe Naomi Marijani kisha kumchoma na magunia mawili ya mkaa, ameomba apewe laini (sim card), zake mbili zenye zaidi ya Sh milioni tano ili awape ndugu zake wakamlipie mwanawe ada.

Mshtakiwa huyo amedai hayo leo Jumanne Agosti 27, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Salum Ally, wakati kesi hiyo ilipotajwa.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amedai upelelezi haujakamilika akaomba kesi iahirishwe.
Kabla ya kuahirisha, mshtakiwa aliomba kuzungumza na mahakama ilimruhusu.

“Mheshimiwa Kituo Kikuu cha Polisi (Central) kuna simu zangu nne lakini katika hizo simu kuna laini mbili ya Tigo na Airtel, zina zaidi ya Sh milioni tano, naomba simu ziletwe mahakamani nihamishie hizo fedha kwa ndugu yangu zikasaidie kumlipia mwanangu ada,” amedai.

Wakili Wankyo alipinga akidai hicho kinachoombwa ni kielelezo hakiwezi kutolewa, lakini anaweza kuandika barua kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) anaweza kumsaidia.


Hakimu Ally alimuagiza mshtakiwa kufuata ushauri wa Jamhuri wa kuandika barua kwa DPP sababu anachoomba ni kielelezo na kesi hiyo haijaanza kusikilizwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles