23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Anayedaiwa kumuua Mwakitwange apata dhamana mahakamani

law

Na MANENO SELANYIKA –DAR ES SALAAM

MAHAKAMA ya Hakimu mkazi Kinondoni jijini Dar es Salaam imempa dhamana Mtafiti wa masuala ya Afya, Glory Anthony (36),anayetuhumiwa kumuua bila kukusudia rafiki yake, Josephat Mwakitwange.

Mahakama hiyo jana ilikubali maombi ya dhamana yaliyowasilishwa na mawakili wa upande wa utetezi.

Uamuzi huo ulitolewa mahakamani hapo mbele ya Hakimu Issa Kasailo.

Upande wa Jamhuri ulikuwa unasimamiwa na Wakili wa Serikali, Matarasa Maharagande wakati upande wa utetezi uliongozwa na mawakili wawili, Godluck Walter na Abdullah Lyana.

Wakili wa Serikali, Matarasa alidai kuwa shauri hilo lipo mbele ya mahakama hiyo kwa ajili ya kutolewa uamuzi mdogo wa dhamana uliowasilishwa na upande wa utetezi.

Wakili Walter aliiambia mahakama hiyo kuwa kulingana na kosa la mteja wake, anaomba apatiwe dhamana kwa sababu  mahakama hiyo ina uwezo huo.

Alisema  Jaji Fauz Twaib wa mahakama kuu kupitia kesi namba 46\ 2012 iliyokuwa inamkabili Elizabeth Michael maarufu Lulu alidhaminiwa.

“Katika kesi hiyo Jaji Twaib alisisitiza kwamba si lazima mahakama kuu itoe uamuzi wa dhamana bali hata za chini zina uwezo wa kutoa dhamana katika kesi ya mauaji bila kukusudia, akitoa mfano wa kesi ya Lulu iliyotolewa uamuzi wa dhamana Juni 11,2011 ,” alidai Wakili Walter.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles