26.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, January 18, 2022

Anayedaiwa kumuua, kumchoma mkewe asomewa mashtaka ya kuua kwa kukusudia

Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Mfanyabiashara Khamis Luwongo (Meshack), anayetuhumiwa kumuua mkewe na kumchoma kwa magunia mawili ya mkaa, amepandishwa kizimbani kwa tuhuma za mauaji ya kukusudia.

Mshtakiwa huyo amepanda kizimbani leo Jumanne saa saba na nusu mchana, mbele ya Hakimu Mkazi, Salum Ally.

Akisomewa mashtaka na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amedai mshtakiwa ni mfanyabiashara, anaishi Gezaulole Kigamboni.

Wankyo amedai mshtakiwa huyo anatuhumiwa kumuua mkewe Naomi Marijani (36), Mei 15 mwaka huu.

Mshtakiwa hakutakiwa kujibu lolote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Upelelezi wa kesi hiyo unaendelea ambapo mshtakiwa amepelekwa gerezani hadi Agosti 13, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
174,926FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles