Anayedaiwa kumuua, kumchoma mkewe afikishwa mahakamani

0
623

Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Mume aliyekuwa akishikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuua mkewe na kisha kumchoma kwa mkaa magunia mawili na kumzika shambani kwake.

Khamisi Luwongo (Meshack), amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumanne Julai 30, ambapo kwa sasa yuko mahabusu akisubiri kupanda kizimbani na kusomewa mashtaka yanayomkabili.


Luwongo amefikishwa mahakamani hapo  saa tatu asubuhi na kuwekwa mahabusu ya mahakama hiyo akisubiri kupangiwa Hakimu.

Hata hivyo, jalada la kesi hiyo ya mauaji ya kukusudia limepangwa kusikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Mmbando.

Mshtakiwa huyo anatuhumiwa kumuua mkewe Naomi Marijani (36), Mei mwaka huu katika maeneo ya Kigamboni jijini Dar es Salaam na kisha kuripoti polisi mkewe huyo ametoweka nyumbani na kwamba amemtumia ujumbe kuwa amemuachia mtoto wake amlee vizuri kwani amechoka na mambo yake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here