32.2 C
Dar es Salaam
Thursday, February 2, 2023

Contact us: [email protected]

Amuua rafiki yake wa kiume kwa bastola

gunNa Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MTU mmoja aliyefahamika kwa jina Joseph Mwakitwange, amefariki dunia baada ya kufyatuliwa risasi kwa bahati mbaya na rafiki yake wa kike aliyetajwa kwa jina la Gloria.

Taarifa za uhakika toka kwa watu wa karibu na Mwakitwange zilizolifikia MTANZANIA Jumamosi, zinaeleza kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kati ya saa nane na tisa wa kuamkia jana.

Kwa mujibu wa taarifa hizo tukio hilo lilitokea katika baa iliyoko Upanga jijini Dar es Salaam ambako Mwakitwange alikuwa na rafiki yake huyo.

“Wakiwa katika baa hiyo, Mwakitwange alitoa pistol yake akaondoa magazine kumbe alisahau tayari kuna risasi ilikuwa kwenye chamber ya pistol hiyo.

“Akampa Gloria amshikie kwa bahati mbaya, Gloria aka ‘pull trigger’ ile risasi iliyokuwa ‘chamber’ ikatoka na kusababisha kifo cha Mwakitwange,” kilieleza chanzo hicho.

Juhudi za gazeti hili kumtafuta Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Christopher Fuime, ili kupata ufafanuzi zaidi juu ya tukio hilo zilishindikana baada ya simu yake kupokelewa na msaidizi wake.

“Ni vigumu kumpata Kamanda Fuime muda huu kwa sababu yupo katika kikao na mimi siwezi kueleza lolote juu ya suala hilo,” alisema.

Taarifa toka kwa watu wa karibu na Mwakitwange, zinaeleza kuwa polisi walifika nyumbani kwake alikokuwa anaishi Mkwajuni kwa ajili ya kufanya uchunguzi.

Inaelezwa kuwa Gloria alikamatwa na polisi na hadi sasa wanamshikilia kwa uchunguzi zaidi.

Baada ya kifo hicho inaelezwa mwili wa Mwakitwange ulikuwa umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala na jana mchana ndugu walikuwa wakifanya taratibu za kuuhamishia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles