26.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

AMUUA MKEWE KWA WIVU WA MAPENZI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari

Na Ibrahim Yassin-Kyela


 

MKAZI wa Kitongoji cha Mikumi Wilaya ya Kyela, Tumbwiza Tweve (43) ameyakimbia makazi yake baada ya kudaiwa kumuua mkewe Hilda Msigwa (34) kwa kumpiga na kitu kizito kichwani kwa madai ya wivu wa mapenzi.

Tukio hilo lilitokea juzi saa nne usiku ambapo mtuhumiwa huyo maarufu kwa jina la kamanda wa wakinga ambaye ni mfanyabiashara wa kuuza nguo minadani alimpiga mkewe kwa nyundo na kutoroka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari amekiri kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema jeshi lake linaendelea na uchunguzi baada ya muuaji kukimbia.

“Jeshi la Polisi linamsaka ili achukuliwe hatua za kisheria na pia nawaomba wananchi kutojichukulia sheria mkononi na badala yake wavitumie vyombo vya sheria pindi unapotokea uhalifu,” alisema.

Majirani waliokuwapo msibani walisema mtuhumiwa na marehemu walikuwa wakigombana kila mara kutokana na mtuhumiwa kumtuhumu mkewe kuwa anachepuka na wanaume wengine.

“Baada ya kumtuhumu mkewe aliweka mtego kwa kumnunulia simu mpya ya kisasa kisha ‘kuiseti’ na kumkabidhi baada ya siku mbili aliichukua na kuifungua.

“Baada ya kuifungua alisikia mazungumzo yote baina ya mkewe na mwanaume mwingine kuhusu mapenzi yao, ndipo mke akakimbilia kwa balozi wa nyumba 10 baada ya kujua ameshtukiwa na mumewe,” alisema mmoja wa majirani hao aliyeshuhudia tukio hilo.

Alisema siku moja kabla ya tukio jioni, mke wa kijana huyo alifika nyumbani kwake akiomba amuombee msamaha baada ya mumewe kugundua mambo yake.

“Baadaye mume naye alifika nyumbani kwa balozi huyo na kumuombea msamaha baada ya mwanamke kukiri ‘kuchepuka’ kisha mume alimsamehe na kuhitaji kurudi naye nyumbani.

“Baada ya kusuluhishwa aliomba abaki na mwanamke kwa ajili ya usalama lakini mwanaume alisema hakuna shida kwa kuwa amekiri amesamehe asubuhi alienda nyumbani kwao kuwataka hali alikuta mlango umefungwa ambapo aligonga dirishani wakaitikia watoto waliosema wamefungiwa mlango kwa nje na baba yao,” alisema.

Alisema aliwaita majirani ambao waliamua kuvunja mlango na kuingia chumba cha wazazi ambapo walisikia mtu akiongea kwa shida ndipo wakakuta mwili wa mwanamke huyo upo chini ya uvungu ukiwa umelowa damu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles