25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Amos Makalla azidi kuiimarika jimboni

Amos MakallaNa Ramadhan Libenanga, Mvomero
MBUNGE wa Mvomero, Amos Makalla, amezidi kuimarika katika siasa jimboni kwake baada ya kuvunja ngome ya Ukawa kwa wanachama 53 wa vyama vya CUF na Chadema kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Tukio hilo lilitokea juzi katika mkutabno wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Madizini, ambako alisema yeye ni mbunge wa vitendo na si wa maneno kama walivyo watu wengine.
Makalla ambaye pia Naibu Waziri wa Maji, alisema katika kipindi alichopewa ridhaa na wapiga kura wake ameweza kuitengeza Mvomero kuwa ya kisasa kuliko ilivyokuwa awali kwa kuhakikisha anayaunganisha makundi yote ya jamii hasa ya vijana, wazee na wanawake.
“Mlinituma kazi na sasa nimeifanya lakini bado naona ndoto na kiu yangu ya kuina Mvomero ikiwa yenye nuru kwa maendeleo kwa watu wote.
“…naitengeneza Mvomero kuwa ya kisasa si kwa ajili ya familia yangu bali ni kwa ajili ya wakazi wote wa bila kujali itikadi za siasa,”alisema Makalla.
Alisema baadhi ya kero za wananchi ambazo mpaka sasa zimetatuliwa ni pamoja na ya maji ambayo mpaka sasa matanki 15 yamejengwa kati ya matanki 20 aliyoahidi.
Alisema kero ya maji katika jimbo lake ndiyo inamnyima usingizi na aliahidi kuimaliza hasa kwa maeneo machache yaliyobaki.
“Yapo maeneo mengi mpaka sasa tumeondoa kero hasa katika sekta ya elimu kwa kusaidia shule za sekondari na msingi kuziimarisha na hata kujenga maabara za kisasa, lakikini pia tumefanikiwa kwenye afya na miundombinu ikiwa si kwa maeneo yote ya jimbo letu.
“Kikubwa ninawaomba ndugu zangu endeleeni kuniamini tuweze kufikia malengo ya pamoja na kuwa na Mvomero ya kisasa zaidi,” alisema Makalla huku akishangiliwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles