29.4 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

AMNESTY: AFRIKA IMESAIDIA KUPUNGUZA ADHABU YA KIFO DUNIANI

LONDON, UINGEREZA


NCHI za kusini mwa jangwa la Sahara zimeimarisha kampeni ya kuondoa adhabu ya kifo baada ya kuchangia katika kupungua kwa utekelezaji wa adhabu hiyo duniani, kwa mujibu wa ripoti mpya ya Shirika la Haki za Binadamu, Amnesty International.

Rpoti hiyo iliyotangazwa jana ilisema kuna mwenendo mzuri unaoendelea duniani, ambapo matukio ya watu kunyongwa yalipungua kwa asilimia nne kutoka watu 1,032 hadi 993 mwaka jana.

Guinea ilifuta adhabu ya kifo kwa makosa yote ya uhalifu, wakati Kenya haitoi tena hukumu ya kifo iliyokuwa ya lazima kwa kosa la mauaji.

Burkina Faso imesifiwa na Amnesty kwa rasimu yake ya katiba ambayo inajumuisha kipengele cha kuondoa kabisa adhabu ya kifo.

Aidha Chad kwa kuanzisha sheria mpya ambayo inaruhusu tu hukumu ya aina hiyo katika kesi ya ugaidi.

Nchi 20 katika eneo hilo zimeondoa adhabu ya kifo kwa makosa yote ya uhalifu, huku Somalia na Sudan Kusini zikiwa nchi pekee zilizotekeleza adhabu hiyo mwaka jana ikilinganishwa na mataifa matano katika mwaka 2016.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles