30 C
Dar es Salaam
Monday, September 27, 2021

Amfuata Lukuvi bungeni kutafuta haki ya ardhi

Ramadhan Hassan -Dodoma   

MKAZI wa Kijiji cha Nyahanga, wilayani Kahama mkoani Shinyanga Magohe Kafumu, amemfuata bungeni jijini Dodoma, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi William Lukuvi, ili amsaidie kupata haki yake ya ardhi hekari 20 alizonyang’anywa na baraza la ardhi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dodoma, alisema lengo lake ni kuhakikisha kuwa anamfikishia kilio chake waziri huyo kutokana na kukosa msaada katika wilaya yake.

Alisema kuwa amekuwa akihangaika kwa muda mrefu kupata msaada katika ngazi tofauti bila mafanikio sasa ameamua kufunga safari na kuja jijini hapa ilia pate fursa ya kuonana na Waziri William Lukuvi.

Alisema eneo analolilalamikia ni la ukubwa wa hekari 20, ambalo alinunua kwa Ilagila Kapagala kwa Sh milioni 3.5 mwaka 2013.

Alisema kabla ya kulinunua eneo hilo alikuwa akikodi kwa mwaka kwa gharama ya Sh  200,000 lakini baadaye mmliki wa eneo hilo akadai kumuuzia.

“Aliposema kuwa anauza nikamuuliza shilingi ngapi akasema kwasababu nimekuwa nikodi basi nimpatie shilingi milioni 3,500,000 nikaanza kumpatia kwanza milioni moja na baadaye mkewe akaja kuifuata fedha nyingine na tulikuwa tukiandikisha kwa mwenyekiti wa kijiji na nakala zote zipo,”alisema

Aidha mara baada ya kulinunua na kuanza kulima alipata wito wa Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya ya Kahama ambapo alikwenda kuitikia wito.

Alisema alipofika katika baraza la ardhi aliiambiwa hatakiwi kufanya chochote kile katika eneo hilo ambalo tayari alishalima mpunga na kutumia gharama kiasi cha Sh milioni 17.3

“Hukumu wakatoa wao kuwa natakiwa kuliachia shamba na mpaka mwezi Juni, mwaka huu natakiwa kutoa vitu vyangu lakini kinachonekana hapa ni kuna watu wanalitaka eneo lile tena kwa bei ya juu na ni viongozi wakubwa wa wilaya yetu,”alisema Kafumu.

Akizungumza kwa njia ya simu aliyekuwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyahanga, Daudi Samsoni alisema katika uongozi wake alishuhudia sehemu ya mauziano ya eneo hilo na kudai kuwa ushahidi wote anao.

“Mimi nikiwa kiongozi sehemu ya mauziano nilishiriki kama mwenyekiti lakini nashangaa kwanini sisi kama mashahidi hatujaitwa na mlalamikaji hakuwahi kwenda katika kesi lakini maamuzi yametolewa,”alisema Samsoni.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi Wilaya ya Kahama, Paulo Lekamoy, alisema kama kuna mtu anaona kuwa haki haikutendeka akate rufaa au aende kokote anakoona kutamsaidia.

“Kama amekuja hapo na anadai anataka kwenda kwa waziri mwache aende na kama hajaridhika na maamuzi basi akate rufaa sina maneno mengine ya kusema nina kazi nyingi za kufanya,” alisema

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,348FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles