25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, December 9, 2023

Contact us: [email protected]

Ame Ali kusaka makali Chalenji

AME-3NA ZAINAB IDDY

MSHAMBULIAJI wa timu ya Azam FC, Ame Ali ‘Zungu’, amesema ana imani kubwa na michuano ya Kombe la Chalenji yanayofanyika nchini Ethiopia kuanzia leo yatamrudisha kiwango chake.

Ame amejiunga na Azam katika usajili wa msimu huu kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro, baada ya kuonyesha umahiri wa kufumania nyavu msimu uliopita akiwa amefunga mabao tisa.

Tangu kujiunga kwake na Azam ameonekana kupotea katika ramani ya soka baada ya kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha kocha Stewart Hall na hata pale inapotokea kupewa nafasi bado haonyeshi kiwango bora kama alivyokuwa Mtibwa.

Akizungumza na MTANZANIA Jumamosi, Ame alisema kupata nafasi ya kuitumikia timu ya taifa ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’, ni nafasi nzuri kwake kurejesha ubora wake wa zamani kwa kuwa atakutana na changamoto nyingi kutoka katika timu mbalimbali na wachezaji wapya.

Alisema anaamini baada ya kurejea katika kikosi chake atakuwa Ame mwingine tofauti na ilivyokuwa sasa.

“Nimekuwa sina nafasi ndani ya Azam kutokana na kocha kutoridhika na uwezo wangu, hivyo nafasi niliyopata katika timu ya taifa ya Zanzibar nitaitumia vizuri kuhakikisha ninakuwa na faida nayo kwa kuongeza kiwango changu na nikirejea ndani ya timu yangu naweza kuwa mpya tofauti na nilivyokuwa awali,” alisema Ame.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles