27.5 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

AMCOS Simiyu zatakiwa kuchangamkia fursa ya mikopo nafuu kutoka NMB

Na Derick Milton, Meatu

Wakati Serikali ikizitaka taasisi za kifedha yakiwemo mabenki kupunguza riba ya mikopo yake kwenye sekta ya kilimo kutoka asilimia 17, Benki ya NMB imeanza kutekeleza maagizo hayo kwa vitendo.

Kupitia Tawi lake la Mwanhuzi lilipo katika Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu, benki hiyo imewakopesha wakulima wa Chama cha Msingi cha Ushirika Meatu Organic Cotton (MOCS –Amcos) mkopo ambao uwawezesha kununua treka mbili kwa ajili ya kuwasaidia wakulima kuandaa mashamba wakati wa kilimo.

Mwenyekiti wa Halmashuari ya Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu, Anthony Philipo akikata utepe wa kukabidhi trekta mbili aina ya Swalaj 885 zilizonunuliwa na Chama cha Msingi cha Ushirika Meatu Organic Cotton (MOCS –Amcos) kwa thamani ya Sh milioni 86 baada ya Chama hicho kupata mkopo wenye riba nafuu kutoka Benki ya NMB. (Picha na Derick Milton).

Katika hafla ya kukabidhi trekta hizo, kwa niaba ya Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Mkoa (Amcos) iliyofanyika Machi 23, mwaka huu, Kaimu Mrajisi Msaidizi, Billwater Mbilinyi amezitaka Amcos nyingine katika mkoa huo kuchangamkia fursa hizo.

Mbilinyi amesema kuwa Benki ya NMB imekuja na mikopo katika sekta ya kilimo yenye riba nafuu ya asilimia 10, kutoka asilimia 17 ya mwanzo, ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya serikali.

Mbilinyi alisema kuwa kwa muda mrefu serikali imekuwa zikitaka taasisi za kifedha kupunguza riba hasa kwenye kilimo ili wakulima waweze kunufaika na kilimo chao, ambapo benki ya NMB imekuwa ya kwanza.

Amesema kuwa fursa hiyo siyo ya kukosa kwa Amcos zote za mkoa wa Simyu, kwani nyingi zina uwezo mkubwa wa kifedha ambapo zinaweza kukopa fedha kujenga maghala ya kuhifadhia mazao pamoja na kununua pembe jeo.

“Meatu Organic Cotton (MOCS –Amcos) hiki chama cha msingi cha Ushirika ambacho kinatakiwa kuigwa na wengine, leo wamenunua trekta mbili baada ya kupata mkopo huu na watarejesha kwa miaka mitatu,” amesema Mbilinyi.

Amesema wakulima wa Amcos hiyo hawataangaika tena kuandaa mashamba yao kwa jembe, bali watatumia trekta hizo ambazo viongozi wa chama chao wamekopa kwa ajili ya kuwasaidia.

Akizungumzia mkopo huo Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, Mulisu Ngassa amesema…“Benki ya NMB imetupatia mkopo wa Sh milioni 77.8 ikiwemo na riba yake, ambapo mkopo huo tumepewa muda wa miaka mitatu kurejesha na kila mwaka tutakuwa tunarejesha kidogo kidogo.

“Mkopo halisi toka Benki ya NMB ni Sh milioni 64.5 na riba yake ni Sh mlioni 13 na tutarejesha Sh milioni 77.8, awali Amcos ilitoa pesa taslimu kama malipo ya awali ya kununua trekta hizo Sh mlioni 21.5, ambazo tumenunua kwa Sh milioni 86,” ammesema Ngassa.

Yohana Mazanzaga ni Mjumbe wa Amcos hiyo ambaye amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan na viongozi wa serikali kwa kufanya ushawishi mkubwa kwenye benki kubwa ikiwemo NMB kuhakikisha zinapunguza riba kwenye sekta ya kilimo.

Mazanzaga amesema kupitia mkopo huo ambao umewawezesha kununua trekta mbili, wakulima wa chama hicho wazalisha kwa kiwango kikubwa kwani hatua hiyo imewezesha kuondoka na jembe la mkono.

“Tunamshukuru sana Rais wetu Mama Samia kwa jitiada zake ambazo zimefanya sasa wakulima tunaweza kupata mikopo kwa riba nafuu, tunawashukuru pia NMB kuwa Benki ya kwanza kutekeleza jambo kwa vitendo…leo tumepata trekta wakulima sasa wanaondokana na jembe la mkono,” amesema Mazanzaga.

Meneja wa Benki ya NMB Wilaya ya Meatu, Waziri Mchalala amewapongeza viongozi wa Amcos hiyo kwa kuchangamkia fursa ya mikopo yenye riba nafuu katika sekta ya kilimo huku akizitaka Amcos nyingine kuiga mfano huo.

“Benki ya NMB inataka kukuza sekta ya kilimo, ndiyo maana imepunguza riba hadi kufikia asilimia 10, tunawaomba wakulima wote katika mazao yote waje mikopo ipo na tutawakopesha kwa ajili ya kuendeeleza kilimo chao,” amesema Mchalala.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles