27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, December 7, 2023

Contact us: [email protected]

AMBER ROSE AJIBU MAPIGO KWA 21 SAVAGE

NEW YORK, MAREKANI


MWANAMITINDO maarfu nchini Marekani, Amber Rose, ameonesha jeuri ya fedha kwa kutumia dola 55,000, zaidi ya Sh milioni 121 kumnunulia mpenzi wake saa.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 33, amethibitisha kuwa kwenye uhusiano na rapa 21 Savage mwenye umri wa miaka 24. Awali rapa huyo alitumia kiasi kama hicho cha fedha na kununua zawadi ya saa kwa Amber, hivyo Amber ameamua kujibu mapigo.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Amber aliandika: “Ninamshukuru Mungu kwa kunipa mwanaume huyu ambaye ananionesha mapenzi ya kweli. Kuna wakati najikuta nadondosha machozi kutokana na upendo wake.

“Sina cha kumfanyia kwa kile anachokifanya kwangu, lakini nimeamua kununua saa kama aliyonipa zawadi na mimi nimemzawadia,” aliandika Amber Rose.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles