22.9 C
Dar es Salaam
Monday, September 9, 2024

Contact us: [email protected]

Amber Rose adondokea kwa mcheza kikapu

amber roseATLANTA, GEORGIA

MWANAMITINDO Amber Rose ameendelea kuzungumziwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari nchini Marekani, baada ya kuonekana na nyota wa kikapu wa timu ya Toronto, Terrence Ross wakiwa katika mazingira ya kimapenzi.

Amber Rose mwenye umri wa miaka 32, amenaswa akiwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, anayecheza katika Ligi ya NBA nchini humo.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, mrembo huyo alidai kwamba amechoshwa na usumbufu wa wasanii wa hip hip, hivyo ni bora atoke na wanamichezo wa kikapu.

“Haya ni maisha yangu mapya na nipo huru kufanya mambo nitakavyo, ukweli ni kwamba wasanii wa hip hop wanachosha, bora niwe na wanamichezo nione itakuwaje,” aliandika Amber Rose.

Mrembo huyo aliwahi kutoka na rapa Kanye West, walipoachana alidondokea kwa rapa mwingine, Wiz Khalifa wakapata mtoto waliyempa jina la Sebastian na sasa amedondokea kwa mcheza kikapu huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles