AMBER ROSE, 21 SAVAGE WANAVYOWABUSTI WOLPER, BROWN

0
640

Na CHRISTOPHER MSEKENA

BAADA ya kuvunjika kwa uhusiano wake na Harmonize, staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe ametua kwenye dimbwi zito la mapenzi kwa mwanamitindo maarufu kwa jina la Brown.

Baada ya kuachana na Harmonize ambaye yupo mapenzini na Mzungu aitwaye Sarah, Wolper alikaa kimya kwa muda mfupi mpaka hivi karibuni alivyoanza kuonyesha uwepo wake kwenye ulimwengu wa mapenzi.

Wiki hii Wolper na Brown wamekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii kwa picha zao zilizowagawa watu katika mafungu mawili makubwa.

Fungu la kwanza ni lile lililojaa mashabiki zake ambao uhusiano huo mpya umewafurahisha na kundi la pili ni lile lililoponda penzi hilo kwa kigezo cha umri.

Kama ilivyo kawaida ya mrembo huyo huwa hafanyi siri pale anapokuwa kwenye uhusiano mpya. Amekuwa akiweka wazi maisha yake ya mapenzi na kutoa nafasi kwa mashabiki kutoa maoni yao.

Wolper amewavuruga mashabiki hasa wale ambao hawapo makini baada ya kuweka video ya mwanamitindo wa Marekani, Amber Rose akipeana mabusu na mpenzi wake mpya rapa mdogo kutoka Atlanta Georgia, Shayaa Bin Abraham Joseph maarufu kama 21 Savage.

Kilichowachanganya zaidi mashabiki ni pale waliposhindwa kumtofautisha rapa 21 Savage na Brown. Kwa kutambua kuwa amewapiga chenga wadaku wanaofuatilia maisha yake ya mapenzi, staa huyo wa filamu aliandika: “Mnajikuta mnaziweza Insta, kumbe hata watu hamuwajui hatari kumbe bff wangu kafanana na 21?”

Usipokuwa makini kumtazama mpenzi wa Wolper yaani Brown na rapa 21 Savage ni lazima utawachanganya kwani wanafanana vitu vingi kama mwonekano, kimo, michoro ya mwilini na huenda umri pia wakawa wanafanana kitu kilichowachanganya mashabiki.

Unaweza kuona ni namna gani Wolper anautumia uhusiano wa Amber Rose na 21 Savage kuyapa nguvu mapenzi yake na Brown.

Anatumia picha na video za Amber Rose akiwa na 21 Savage kufananisha na uhusiano wao. Amber Rose anasema 21 Savage ni mwanamume wa maisha yake, hajali utofauti wa miaka 9 aliyomzidi maana mrembo huyo ambaye amezaliwa mwaka 1983 na rapa huyo amezaliwa mwaka 1992.

Anachokifanya Wolpe ambaye alizaliwa 1987 kwa mpenzi wake Brown, ndiyo anachokifanya Amber Rose kwa mpenzi wake, 21 Savage.

Tangu uhusiano wao uwe wazi, Amber Rose amekuwa akimmwagia maneno matamu laazizi wake huyo kwenye mitandao ya kijamii hali kadhalika Wolper anafanya hivyohivyo kwa Brown.

Mfano hivi karibuni, Amber Rose aliweka wazi hisia zake za mapenzi kwa 21 Savage kwa kuandika: “It’s pretty amazing waking up every morning feeling love like this.”

Maneno hayo yaliambatana na picha inayomwonyesha akiwa na mpenzi wake huyo katika pozi matata.

Wolper naye katika moja ya picha aliyoiweka wiki hii akiwa na mpenzi wake huyo alichombeza kwa maneno: You are amazing and don’t forget it #Bff.

Mrembo huyo ameendelea kuonyesha imani na mahaba makubwa kwa mwanamitindo huyo ambaye naye amerudisha upendo kwa kuchora tattoo juu ya kifua chake inayosomeka I love Wolper.

Ndiyo mambo ya mastaa hayo. Penzi la Amber Rose huko majuu, linakuja kuakisi penzi la Wolper hapa Bongo. Muhimu ni upendo wa kweli na isije kuwa ni script kama zile wanazokariri wakiwa mbele ya kamera wakati wakirekodi filamu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here