AMBER LULU, GIGY MONEY LAO MOJA

0
1835

NA JESSCA NANGAWE


MREMBO anayefanya vyema kwenye tasnia ya burudani hapa Bongo, Lulu Euggen maarufu kama Amber Lulu, amesema moja ya malengo yake kwa sasa ni kuitwa mama kama ambavyo rafiki yake wa karibu, Gigy Money, alivyoamua.

Akizungumza, Amber Lulu, amesema sasa amekuwa mtu mzima anayeweza kufanya maamuzi yake sahihi hivyo anachotamani kuona kwa sasa ni kuitwa mama kama baadhi ya mastaa wenzake walivyofanya maamuzi.

“Mtoto ni jambo jema, ukiangalia wasanii wengi sasa wamekuwa na maamuzi ambayo mimi nayaita ni sahihi, Gigy Money wakati wowote ataitwa mama, hii inafariji sana hata mimi amenipa moyo wa kufanya hivyo, naamini majaliwa ya Mungu yakifika hili litafanikiwa,” alisema Amber Lulu.

Alisema mtu sahihi wa kuweza kupata naye mtoto kwa sasa ni mpenzi wake Prezzo ambaye ni mwanamuziki mwenzake kutoka  Kenya.

Kwa sasa Amber Lulu anafanya vyema na kibao chake cha ‘Jini Kisirani’.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here