Amber Lulu awafumbua wasanii

0
780

Glory Mlay

MSANII Amber Lulu, amewataa wasanii kujitambua na kuwekeza katika biashara nyingine ili kujipatia kipato zaidi.

Amber Lulu amesema kuwa muziki unalipa lakini hauwezi kukufikisha kwenye malengo makubwa ambayo umejiwekea.

“Wasanii tujitambue na tujifunze kuwekeza katika biashara nyingine, maisha yamekuwa magumu na ukiangali wengi hatujafika kwenye malengo ambayo tunayahitaji, hivyo ukitegemea muziki pekee hatuwezi kutoboa,” alisema.

Mbali na hilo, Amber Lulu aliwataka wasanii kujikinga na maambukizi ya Corona kwasababu umekuwa janga kwa taifa na duniani kote.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here