22.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

AMBER LULU ATOBOA SIRI YA MASTAA KUOA NJE

NA JESSCA NANGAWE


VIDEO vixen maarufu wa Bongo, Lulu Mkongwa maarufu kama ‘Amber Lulu’, amesema kitendo cha mastaa wa Bongo kukimbia kuoa nje ni jinsi wanawake wengi wa hapa walivyojiweka na kuridhika kimaisha.

Amber Lulu ambaye naye yupo mbioni kuolewa na staa wa Kenya, Prezzo, amesema inabidi maamuzi ya kila mmoja kujichagulia maisha yaheshimiwe kwa kuwa hakuna anayeweza kumpangia mwenzake jinsi ya kuishi.

“Mimi nakubaliana na maamuzi yao, unajua mapenzi hayaingiliwi, hata mimi hivi karibuni nahamia Kenya, nadhani pia wanawake wengi wa Bongo tumeridhika na mafanikio madogo, hatutaki kuangalia mbali, kwa hiyo mtu anafanya maamuzi kwa ajili ya maisha yake ya baadaye,” alisema Amber Lulu ambaye kwa sasa anafanya vyema na ngoma ya ‘Jini Kisirani’.

Miongoni mwa mastaa waliofanya uamuzi wa kuoa nje ya Tanzania ni pamoja na Ambwene Yesaya ‘AY’, Ali Kiba, Fid Q, huku wanaotarajia kufanya maamuzi kama hayo ni pamoja na Harmonize pamoja na Stamina.

Aliongeza kuwa kwa sasa yeye na mpenzi wake Prezzo wana mikakati mingi kubwa ni kuona jinsi ya kupanga familia yao baada ya kila mmoja kuridhika kuishi na mwenzake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles