25.5 C
Dar es Salaam
Monday, November 29, 2021

Ambaka mtoto wa miaka 14 na kumchana mfuko wa uzazi

TWALAD SALUM, MWANZA

MKAZI wa Kijiji cha old Misungwi wilayani Misungwi Mkoani Mwanza, Mashaka Elias (25), amefikishwa katika mahakama ya wilaya hiyo kwa tuhuma ya kubaka mtoto wa miaka 14 na kumchana mfuko wa uzazi.

Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Ramsoney Salehe, akisoma hati ya mashitaka ya kesi hiyo namba 32 ya mwaka 2020, alidaiMachi tatu mtuhumiwa alimbaka mtoto huyo mwenye miaka 14 kinyume cha sheria.

Salehe alidai mtuhumiwa alikutana na mtoto huyo na kumtaka waende nyumbani kwake akachukuwe fedha ya mzazi wake.

Alidai mtoto huyo alikataa na kusema alikuwa na haraka kwenda nyumbani lakini baadaye kubali kumfuata mtuhumiwa ambapo wakiwa njiani kabla ya kufika nyumbani kwake, alimshika na kumlaza chini na kumbaka.

Alidai mahakamani hapo kwamba, aliyefanyiwa kitendo hicho bado yuko hospitali akipatiwa matibabu kwasababu mfuko wa uzazi ulichanika wakati akibakwa.

Kutokana na hali hiyo, aliiomba mahakama kutotoa dhamana kwa mtuhumiwa kwani upande wa mashitaka haujakamilisha upelelezi.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa wilaya hiyo, Eric Marley aliahilisha kesi hiyo hadi March 17 ambapo mtuhumiwa  atasomewa maelezo ya awali.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,301FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles