22.8 C
Dar es Salaam
Saturday, June 3, 2023

Contact us: [email protected]

Amana Bank yazindua Programu ya kidigitali inayowezesha huduma za Kiislamu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Wakati taasisi za kifedha zinaendelea kubadilika na kurahisisha huduma na njia ya kufanya biashara, Amana Bank imetangaza kuzindua programu yake mpya ya kidigitali ijulikanayo kama Amana Bank App ambayo itawawezesha wateja kufanya miamala mtandaoni.

Wateja wa Amana Bank wakipatiwa maelezo ya matumizi ya teknolojia hii mpya ya kidigitali wakati wa hafla ya uzinduzi

Amana Bank Limited, inayoongoza kwa kutoa huduma za Kibenki za Kiisilamu nchini Tanzania,  leo Jumanne Julai 27, 2021 imetangaza kuwa imefanya mapinduzi ya huduma zake za kibenki kupitia simu za mkononi kwa kuanzisha programu mpya kupitia simu za mkononi, inayomwezesha mteja kufanya malipo na huduma za kibenki kwa wateja wake iitwayo Amana Bank App.

Kwa mujibu wa benki hiyo, Programu hiyo inawezesha kupata huduma za kibenki kidigitali kama vile kufanya malipo, kuhamisha fedha, kulipa bili  na kufanya malipo mtandaoni, kupokea taarifa za benki na kupokea habari juu ya huduma zinazotolewa na benki kama mikopo, viwango vya ubadilishaji wa kigeni na hata kulipia huduma mbalimbali kama malipo ya serikali na huduma za bima.

Amana Bank App pia ni huduma inayoweza kutumika kwa malipo: Inawezesha mteja kuchanganua (ku scan) namba yake ya Masterpass QR na kulipia huduma mbalimbali ikiwemo kulipia mafuta ya gari, maduka ya vyakula, migahawa, maduka ya dawa, hospitali, vituo vingi  vinavyotoa huduma.

Programu ya Amana Bank App imebuniwa kuhudumia wateja ambao wanahitaji kuweka fedha zao kwa kufuata mwongozo/kanuni wa huduma za kibenki za Kiislamu. Programu ya Amana imebuniwa kama daraja jipya la kuwaunganisha  wateja ambao wanahitaji huduma ya kibenki ya Halal, ambapo wataweza kufungua akaunti ya akiba ya Amana Bank kwa njia ya kidigitali na papo hapo.

Akiongea juu ya ubunifu huu, Mkuu wa Masoko wa Amana Bank, Dassu Mussa,  alisema,

“Amana Bank daima imekuwa mstari wa mbele kuanzisha ubunifu unaowezesha wateja kuchagua huduma wanazohitaji zinaongozwa na kanuni za Kiislamu. Aliongeza kuwa kwa msingi huu tulikuwa wa kwanza nchini kuanzisha huduma ya kuweka fedha ya Halal kwa njia ya kidigitali mnamo mwaka  2018,” amesema Mussa na kuongeza kuwa huduma inawezesha wateja kuweka fedha kupitia simu zao za mkononi na kupata faida kwendana na kanuni za Hilal.Ubunifu huu umelenga kuhakikisha unaongeza ujumuishaji wa huduma za kifedha kwa wananchi kupitia huduma zake ambazo zinafuata misingi ya Sharia. 

Huduma nyingi zitaongezwa hivi karibuni: Orodha ya huduma zinazokuja za kusisimua ni pamoja na  kuomba mikopo kutumia programu za simu,kutoa kadi za zawadi na nyinginezo nyingi.

Alitaja zaidi huduma zingine zinazotolewa na benki hiyo kuwa ni huduma ya benki kupitia  simu inayoweza kupatikana kwa kupiga * 150 * 12; Amana Bank Mastercard ambayo inaruhusu wateja kutoa pesa kutoka mahali popote ulimwenguni; Virtual Card inayoweza kupatikana kupitia Programu ya Simu ya Mkononi na inawezesha kufanya mihamala ya malipo kwa njia ya mtandao kupitia kadi zao  za Mastercard  na Mawakala wa Benki ambapo wateja wanaweza kufanya miamala, kufungua akaunti na kulipa bili kupitia vibanda vya wakala wa Amana vilivyopo mitaani.

Ili kupakua App ya Amana, nenda tu kwenye programu ya simu ya   Playstore (Android) au Appstore (IOS), tafuta Amana Bank App, kisha upakue programu hiyo, bonyeza kitufe cha kujiunga, soma, na ukubali maelezo, ingiza nambari ya akaunti yako, nambari ya simu na nywila unayotumia kwa Amana Banking yako (USSD * 150 * 12 #). Kisha utapokea SMS yenye namba maalum  ambayo itakubidi uweke kwenye kisanduku kinachohitajika kisha bonyeza kitufe cha kuambatana na kufuatiwa na nywila yako mwishowe kupokea orodha ya Programu ya Amana Bank.Ingawa, kutumia App hiyo, lazima mteja awe na akaunti na Amana Bank AU ungana na huduma ya Amana Banking kupitia USSD * 150 * 12.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,270FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles