27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 4, 2023

Contact us: [email protected]

AMA KWELI CCM NI ILE ILE

CCMKUNA  wakati  mambo mengi yanatokea lakini mengine yalishasemwa awali kuwa yatakuja kutokea ila kipindi yanasemwa ilikuwa ni vigumu kudhani kama jambo hilo litakuja kutokea na mengine  tunaambiwa lakini watu wanaofikisha ujumbe  si rahisi kwetu sisi kuamini kuwa wanaweza wakasema lolote baya kuhusu kitu fulani ni kama vile ambavyo hatuamini kuwa shetani anaweza kutuletea habari za kuokoka ili tuuone ufalme wa mbingu.

Moja kati ya mambo yaliyosemwa ambayo tusingeweza kudhani kuwa ujumbe ule tulikuwa tunafikishiwa sisi na si kujiburudisha kama tulivyodhani basi ni ule wimbo wa bendi ya Chama Cha Mapinduzi Tanzania One Theatre (TOT) unaofahamika  ‘wacha waisome namba…. CCM mbele kwa mbele’

Kwenye huu wimbo vimeimbwa vitu vingi lakini moja kati ya mashairi ambayo ukiyafikiria mara mbili huwezi kupata picha kamili kwa nini mwandishi wa wimbo huu aliamua kuimba vile ni ule mstari usemao ‘CCM ni ile ile’. Huu mstari kila nikiutafakari haiji maana nyingine yoyote zaidi ya kudhani kuwa hakuna mabadiliko yoyote yanayoweza kutokea chini ya CCM kitu ambacho ni ngumu kuamini kuwa mwandishi wa wimbo huo alimaanisha hivyo.

Kwa nini CCM ni ile ile?

Hebu tujikumbushe maneno haya kwanza kutoka kwa Mheshimiwa  Rais John Pombe Magufuli  “Unakuta mtu kaharibu Tarime anapelekwa Mwanza, akiharibu Mwanza anahamishiwa Tanga, kwenye Serikali yangu hakutakuwa na utaratibu mbovu kama huo, ukiharibu sehemu moja ujue umeharibu maisha yako yote, kwangu ni kazi tu, ukiondoka umeondoka hakuna kuhamishwa” Hayo yalikuwa ni maneno ya Mheshimiwa Rais kipindi cha kampeni sasa tuulizane wote hapa je, CCM si ile ile?

Serikali aliyodai ilikuwa ikihamisha watu ikamaliza muda wake ikaja Serikali ya Awamu ya Tano ambayo iliahidi kutohamisha watu wanaoharibu nayo inahamisha vile vile kama ilivyohamisha Serikali ya Awamu ya Nne aliyoituhumu, Je CCM si ile ile?

Paukwa pakawa ikawa siku yakasogea masaa ikazidi kuripotiwa kuwa kuna watumishi wameharibu mahala fulani tukashuhudia taarifa zao kwenye vyombo mbalimbali lakini kila walipotangazwa kuondolewa kwao tukasikia kuwa watatafutiwa kazi nyingine za kufanya tukajiuliza kwa nini watafutiwe kazi nyingine wakati tuliambiwa awamu hii hakutakuwa na utaratibu huo ila kabla ya siku nyingi kupita tukasikia watu wamepangiwa kazi nyingine, Je, bado hatuuamini ule wimbo kuwa CCM ni ile ile? Au kwa kuwa wimbo ule ulitungwa na bendi yao?

Kwenye utatuzi wa tatizo fulani au ukiwa unatafuta njia ya kupata ufumbuzi wa jambo fulani wataalamu husema kufahamu tatizo ni moja kati ya njia ya kupata ufumbuzi wa kulitatua hilo janga lakini wataalamu hao hao huhimiza kuwa ukilifahamu kosa au chanzo cha tatizo na ukirudia kosa lile lile unakuwa unafanya kosa kubwa zaidi,  Rais alifahamu fika kuwa hapa nchini kuna tatizo na hakuishia hapo bali alifahamu na chanzo cha tatizo na akaahisi kuwa atalitafutia ufumbuzi lakini baada ya kulitatua naye ameingia kwenye mkondo ule ule aliopita mtangulizi unafikiri kuna tatizo lingine zaidi ya kusema Ccm ni ile ile?

Kuahidiwa na kuachwa njia panda hiyo ni kawaida kwa CCM na tuliambiwa hivyo kwenye ule wimbo kuwa CCM  ni ile ile, leo hii tunashangaa inakuwaje mmoja wa wanachama maarufu waCCM anateuliwa tena na wakati ni miezi michache nyuma alitumbuliwa kisa alishindwa kukabidhi idadi ya watumishi hewa alipokuwa mkuu wa mkoa fulani.

Ama kweli nimeamini CCM ni ile ile.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles