23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

ALMASI ZAWAFIKISHA VIGOGO WAWILI KORTINI

PATRICIA KIMELEMETA NA MANENO SELANYIKA

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imempandisha kizimbani aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa tathmini wa Wizara ya Nishati na Madini, Archard Kalugendo (49) na mwenzake na kumsomea shtaka moja la uhujumu uchumi na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh bilioni 2.

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage, Wakili wa Serikali, Paul Kafushi, alimtaja mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni Edward Rweyemamu (50),  ambaye ni mthamini wa madini wa Serikali.

Alidai kuwa washtakiwa hao walitenda kosa hilo kati ya Agosti 25 na 31, mwaka huu maeneo mbalimbali kati ya Dar es Salaam na Shinyanga.

Alidai kwa pamoja wakiwa kama wathamini wa madini ambao wameajiriwa na Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, walisababishia hasara Serikali dola za Marekani 1,118,291.43 ambazo ni sawa na Sh 2,486,397,982.54.

Alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuiomba mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hata hivyo, Hakimu Mwijage alisema kwamba shtaka linalowakabili washtakiwa hao halina dhamana na kwamba mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo hadi mahakama kuu.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 29, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na watuhumiwa walirudishwa rumande.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles