23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Ally Mayay akubali kukatwa TFF

Na Winfida Mtoi, Mtanzania Digital

Aliyekuwa mgombea wa urais wa Shirikisho la Soka Tanzania, Ally Mayay, amekiri kuwa amestahili kukatwa katika kinyang’anyiro hicho kutokana na kutofikisha idadi ya wadhamini watano walitakiwa.

Mayay na mwanahabari Osca Osca ni kati ya wagombea walienguliwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa madai ya kushindwa kukidhi vigezo vya kikanuni.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mayay amefafanua kuwa aliwasilisha vitu vyote vinavyotakiwa ikiwamo vyeti lakini upande wa wadhamini hawakukamilika.

“Kati ya vitu vilivyotakiwa kuwasilishwa kwenye kama ni kitambulisho cha uraia, vyeti vya shule na barua za wadhamini watano, lakini mimi nimepata mdhamini mmoja,” amesema Mayay.

Ameeleza kuwa amejitahidi kuomba udhamini katika klabu zote 18 za Ligi Kuu Tanzania Bara ila mmoja ndiye alimuunga mkono.

Amesema kuenguliwa kwake katika uchaguzi huo hakutamfanya aache kutoa mchango wake kwenye soka, ataendelea kama alivyokuwa.

“Nitaendelea kutoa mchango katika soka kwa nafasi nilikuwa nayo, pia nipo tayari kutoa ushauri kwa wagombea wakihitaji sera zangu nilizotakiwa kuwasilisha kipindi cha kampeni,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,226FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles