27.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, January 18, 2022

Alliance wamvuruga Minziro

Zainabu Iddy, Dar es salaam

KOCHA Mkuu wa timu ya Singida United, Felix Minziro, amesema kuwa kitendo cha uongozi wa Alliance FC kusitisha mechi yao ya kirafiki kimemvurugia programu zake.

Singida United na Alliance FC zilipanga kucheza mechi ya kirafiki Jumamosi iliyopita, lakini siku moja kabla ya mchezo Alliance wakawapa taarifa kuwa timu yao haitacheza mechi hiyo.

Akizungumza na MTANZANIA, Minziro alisema kuwa kitendo hiko kimemvurugia mipango yake kwa sababu alihitaji kujua kama mapungufu yaliyojitokeza kwenye mechi zilizopita yamemalizika au laa.

“Kila mwalimu ana mipango yake pale anapojua kuna mechi mbele yake, binafsi kuna vitu nilitaka kuviangalia kwenye kikosi changu kama tungecheza na Alliance, lakini mambo yamevurugika.

“Kutokana na hilo, itanibidi nitafute timu nyingine ya kucheza nayo kabla ya kuanza safari ya kwenda Shinyanga kucheza mchezo wetu wa kwanza wa ligi dhidi ya Mwadui FC,” alisema.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
175,086FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles