31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Aliyemmwagia sheha tindikali akamatwa

Mohammed Omar Saidi Kidevu
Sheha wa Shehia ya Tomondo mjini Zanzibar aliyemwagiwa tindikali, Mohammed Omar Saidi Kidevu

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

MAKACHERO wa Jeshi la Polisi Zanzibar wamefanikiwa kumtia mbaroni mmoja wa washukiwa wa matukio ya tindikali visiwani hapa, Alawi Mohammed Silima (25), mkazi wa Fuoni Melinne.

Ofisa Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Inspekta Mohammed Mhina, alisema mtuhumiwa huyo anahusishwa na tukio la kummwagia tindikali Sheha wa Shehia ya Tomondo mjini Zanzibar, Mohammed Omar Saidi Kidevu, kabla ya kutoweka Mei 23, mwaka jana.

Alisema mtuhumiwa huyo ambaye muda mrefu alikuwa akisakwa na polisi kwa tukio hilo, alikamatwa juzi usiku akiwa mafichoni katika eneo la Fuoni, baada ya taarifa za kiintelijensia kubaini kuwepo kwake.

“Bado makachero wanaendelea kumhoji mtuhumiwa huyo kwa lengo la kuubaini mtandao mzima wa matukio mbalimbali, yakiwemo ya tindikali yaliyotokea siku za nyuma visiwani humo,” alisema Mhina.

Alisema kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kunatokana na taarifa za siri za raia wema ambapo Jeshi la Polisi lilikuwa likiendelea na upelelezi wa chini kwa chini wa kumbaini mtuhumiwa na mahali alipojificha.

Baadhi ya wananchi wa Zanzibar wamepongeza kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na kuliomba jeshi la polisi kuendelea na juhudi zake za kuwasaka watuhumiwa wengine wanaohusika katika matukio mengine kama hayo siku za nyuma visiwani hapa.

Tukio la kumwagiwa tindikali kwa sheha huyo lilitokea Mei 22, mwaka jana saa 2.45 usiku, wakati alipokuwa akirudi nyumbani akitoka kuchota maji nyumba jirani.

Sheha huyo alijeruhiwa vibaya mgongoni, kifuani, sikio na jicho la upande wa kulia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles