26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

ALIYEMKASHIFU MTUME Z’BAR KUFIKISHWA KORTINI

Na Muhammed Khamis (UoI)-ZANZIBAR


 

hamdan-omar-makameJESHI la Polisi Zanzibar linatarajia kumfikisha mahakamani mtu anayedaiwa kumkashifu Mtume Muhammad (S.A.W).

Mtuhumiwa huyo, Dk. Abdallah Saleh Abdallah (50), mkazi wa Kikwajuni mjini Unguja, baada ya kutoa maneno hayo ya kashfa juzi na kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Unguja, Kamishna wa Jeshi la Polisi visiwani hapa, Hamdan Omar Makame, alisema walimtia mbaroni daktari huyo wa binadamu baada ya taarifa zake kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, ikiwamo wa Facebook.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kumkashifu Mtume Muhamad na waumini wa dini ya Kiislamu.

“Tumemkamata mtuhumiwa na tayari tumeshakamilisha kila kitu, ikiwamo taarifa za upelelelezi. Hivyo kilichobaki ni kumfikisha makahamani tu ili aweze kujibu mashtaka yake,” alisema Kamishna Makame.

Akiongezea kuhusu ukusanyaji wa taarifa za upelelezi, alisema wamelazimika kumshikilia kijana Ali Juma Makame (30) mkazi wa Michenzani mjini hapa ambaye anatuhumiwa kusambaza video hizo mitandaoni.

“Tunawanasihi waumini wa dini ya Kiislamu kutokubali kuyumbishwa na kufanya maandamano kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na sheria, ni bora kujiepusha na jambo hili kwani tayari vyombo vya ulinzi vimeshachukua hatua kwa mujibu wa sheria,” alisema.

Kutokana na video hiyo, taasisi mbalimbali za dini ikiwamo Jumuia ya Maimamu Zanzibar (JUMAZA) na Ofisi ya Mufti, zimelaani tukio hilo na kutoa wito vyombo vya sheria kuchukua hatua na kufanya kazi bila upendeleo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles