31.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

Aliyemjeruhi rais Brazil agundulika kuwa na matatizo ya akili

RIO DE JANEIRO, Brazil

MAHAKAMA Kuu ya hapa imesema   mwanamume  aliyemshambulia Rais Jair Bolsonaro  Septemba mwaka jana wakati wa kampeini ana ugonjwa wa akili na hivyo hawezi kufungwa.

Jaji    Bruno Savino, alisema juzi kwamba  Adélio Bispo de Oliveira wakati akifanya tukio hilo, alikuwa hawafahamu   alichokuwa anakifanya kutokana na matatizo yake ya akili na hivyo hawezi kufungwa kutokana na kosa hilo.

Awali, Rais  Bolsonaro, ambaye alihitaji kufanyiwa upasuaji baada ya tukio hilo alikuwa akiamini ni masuala ya msukumo wa siasa.

Hata hivyo baadaye polisi walisema  watamfanyia mwanamume huo uchunguzi kuona kama alikuwa na matatizo ya akili, baada ya kuwaeleza kwamba alifanya kitendo hicho kwa maagizo ya Mwenyezi Mungu.

Akitoa hukumu hiyo juzi, Jaji  Savino alisema   alifikia uamuzi huo kutokana na ripoti iliyowasilishwa na wakili aliyekuwa akimtetea De Oliveira.

Katika tukio hilo, Rais  Bolsonaro (64), alinusurika kifo baada ya kupata majeraha makubwa    baada ya kushambuliwa maeneo ya tumbo wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika eneo la  Minas Gerais Septemba mwaka jana.

Mwanasiasa huyo mwenye mrengo wa kulia alilazimika kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kutokana na majeraha hayo ambayo yalisababisha hata mfumo wake wa kumeng’enya chakula kushindwa kufanya kazi hadi akawekewa  mfuko maalum tumboni kabla ya kutolewa Januari mwaka huu.

Rais  Bolsonaro, ambaye alikabidhiwa madaraka ya nchi Januari mwaka huu ni mwanasiasa mtata ambaye wachambuzi wa masuala ya siasa wanamfananisha na Rais wa Marekani, Donald Trump.

Adélio Bispo de Oliveira ni mfuasi wa sera zamrengo wa kushoto ambaye amekuwa akipaza sauti kumshutumu Rais  Bolsonaro, akitumia njia ya ujumbe wa  Facebook kunadi sera zake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles