Aliyemfungia mtoto kabatini atembezewa kichapo

0
1266

Na RAMADHAN HASSAN

-DODOMA

JESHI la Polisi limelazimika kumtia tena mbaroni Anitha Kimaro, ambaye anadaiwa kumfungia kabatini mtoto wa miezi sita.

Hatua hiyo imekuja baada ya wananchi wenye hasira kuvamia nyumbani kwake na kuanza kumtembezea kichapo huku wakipinga hatua ya polisi kumpa dhamana.

Anitha ambaye pia ni mwalimu wa Shule ya Msingi Chadulu mjini hapa, anatuhumiwa kumfanyia ukatili mfanyakazi wake wa ndani (jina linahifadhiwa), kwa kumpiga na kumjeruhi, huku akimfungia ndani ya kabati mtoto wake wa miezi sita Mtaa wa Makongoro, Kata ya Kiwanja cha Ndege.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto alisema waliamua kumkamata tena Anitha kutokana na usalama wake uraiani kuwa mdogo.

Alisema awali walimkamata mtuhumiwa huyo, lakini ilibidi wamwachie kwa dhamana ambayo ni haki yake ya msingi.

“Tulimwachia kwa dhamana, lakini jana (juzi) tulilazimika kumkamata tena kutokana na usalama wake kuwa mdogo baada ya wananchi wenye hasira kuvamia nyumbani kwake,” alisema.

Kamanda Muroto aliitaja sababu nyingine ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kwamba anadaiwa kuharibu …

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here