27.5 C
Dar es Salaam
Sunday, December 3, 2023

Contact us: [email protected]

ALIYEMCHOMA MOTO MWANAMKE MBARONI Z’BAR

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Hassan Nassir Ali.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Hassan Nassir Ali.

Na MUHAMMED KHAMIS (UOI)-ZANZIBAR

POLISI Mkoa wa Mjini Magharibi wamefanikiwa kumkamata mmoja wa watuhumiwa wanaodaiwa kumchoma Samira Abbas Amin (26), ambaye kwa sasa yupo hospitali anaendelea na matibabu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Hassan Nassir Ali, alisema wamefanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa huyo, Omar Said Omar (24), ambaye anadaiwa kuhusika na tukio la kumchoma moto mwanamke huyo katika eneo la Paje, Kisiwani hapa.

Alisema kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kunatokana na mtego waliowekewa na jeshi hilo ambapo walifanikiwa kumtia nguvu katika eneo la Darajani, mjini Unguja.

Kamanda Nassir alisema kwa mujibu wa taarifa za awali ambazo Jeshi la Polisi limezipata, watu hao wawili walikuwa na uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu na walikuwa wakiishi pamoja Paje, kabla ya kutofautiana.

“Tulipokea taarifa mapema kutoka kwa raia wema juu ya kijana huyu na dhamira yake ya kukimbia na ndiyo maana tukaweka mtego kuhakikisha tunamkamata akiwa na dereva wa gari walilokuwa wanatumia aina ya Vits yenye nambari za usajili Z 853 GJ,’’ alisema Kamanda Nassir.

Kutokana na tukio hilo, hali ya taharuki ilitawala jana katika eneo la Darajani miongoni mwa wananchi baada ya askari waliovalia sare maalumu kuonekana wakiwa kwenye doria maalumu, huku wakizunguka eneo la Kituo Kidogo cha Polisi Mkunazini.

Tukio ambalo la kikatili ambalo limevuta hisia za watu kisiwani hapa, limemfanya Mratibu wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Mzuri Issa, kusema licha tukio hilo kuwa baya, lakini jambo la kutia matumaini ni hatua ya Jeshi la Polisi kumtia mbaroni mtuhumiwa ili sheria ichukue mkondo wake.

Alisema vitendo hivyo vya kikatili kutoka Visiwani Zanzibar havileti picha nzuri ambapo aliiomba jamii kupaza sauti kwa kupinga kwa vitendo, ikiwamo kutoa taarifa kwa Polisi ili kukomesha tabia hiyo mbaya.

“Tunaamini kwa hili haki itatendeka, maana ushahidi upo wazi kwa kila kitu, hivyo hatutarajii kuona kesi hii ikibezwa, badala yake tunaamini itakwenda haraka sana na kutolewa hukumu,’’ alisema Mzuri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles