24.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

Aliyekuwa mbunge Mafia afariki dunia

Mwandishi Wetu- Dar es Salaam

ALIYEKUWA  Mbunge wa Mafia mkoani Pwani, Abdulkarim Shah amefariki dunia.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Taifa Gas, Rostam Aziz ilisema Shah alifariki juzi katika Hospitali ya Hindu Mandal.

“Hadi anafariki dunia Jumamosi, mheshimiwa Shah alikuwa Makamu Mwenyekiti a Bodi ya Wakarugenzi wa Taifa Gas,”alisema Rostam

Kuhusu taratibu za msiba na mazishi, alisema zitatangazwa baadaye, baada ya kukamilika taratibu zote.

Enzi za uhai wake,  Shaha  aliwahi kuwa mmoja wa makamishina wa Bunge na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

Alizaliwa eneo la Gerezani mwaka 1961 na kupata elimu msingi mwaka 1969 hadi 1975 katika Shule ya Msingi Muhimbili.

Baadae alipata elimu ya sekondari Shule ya Kinondoni mwaka 1976 na kuhitimu 1979.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

12,054FansLike
2,941FollowersFollow
18,400SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Latest Articles