27 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

ALIPO BARNABA SI LEVO ZAKE KABISA!

Na RAMADHANI MASENGA

KUWA na kipaji ni suala moja, kukitumia ni suala la pili. Ila suala muhimu zaidi ni kuvuna matunda stahiki kupitia kipaji husika.

Ni ujinga kuwa na kipaji na kuishia kupewa sifa tu. Haina maana kuwa na kipaji kikubwa ikiwa wanaofaidika ni wale wenye vipaji vya kawaida.

Barnaba ni msanii mwenye kipaji kikubwa. Wengi wa wasaniii wanaimba leo wanafaa kuwa wanafunzi wake au wasaidizi wake kama angekuwa na bendi.

Miaka miwili nyuma kila mmoja alidhani leo angekuwa mbali sio tu kimafanikio ya kifedha ila labda hata muziki wake usingekuwa unaimbwa Kariakoo na Sinza peke yake.

Thamani na hadhi ya sauti yake inaweza kumshawishi hata mpenda soka akautazama muziki na kuufurahia. Anapiga kinanda, gitaa pamoja na kuichezea sauti yake kama mtoto awezavyo kucheza na mdoli.  

Unapomsikia akiimba ni sawa na kula pilau ya sikukuu. Kila mpenda muziki anamuita mwanamuziki. Mwenye kuujua muziki anamuita Barnaba ni mwanamuzi kamili.

Katika kipaji chake kuna ziada ya kuwa msanii wa Bongo Fleva wa kawaida. Haikufaa Barnaba awe hapa mpaka leo.

Mwaka alioibuka Diamond na kuanza kukamata chati, nyuma yake alikuwa Barnaba. Ilikuwa ni ngumu kutaja wasanii wawili wa juu na kuacha kumtaja Barnaba.

Kuna kitu alionesha anakuja kutufanyia. Tulikuwa tukisubri muda aweze kugeuza redio zetu kuwa za nyimbo zake tu, ila wapi.

Ule muda tulioamini  unafika kwa ajili ya utawala wake unaonekana kama haufiki na zaidi ni kama kuna watawala zaidi yake.

Leo baada ya Diamond huwezi kumtaja Barnaba tena kama zamani. Kutoka kwa Barnaba mpaka umfikie Diamond, hapa kati ni lazima ukutane na wasanii wengine kama watano!

Tena ni wasanii si wanamuziki kama yeye. Ile hadhi na shauku ya watu kuanza kumsikia Barnaba katika dunia tofauti inaonekana kama kufutika na dhana ile kumpa mwingine.

Huwezi kumpa shoo Barnaba ukamosa Ommy Dimpoz. Huwezi kumtaja Barnaba kabla hujasema neno kuhusu Ben Pol kama zamani.

Kuna kitu hakiko sawa kwa Barnaba. Mbali na ukubwa wa kipaji chake pamoja na uwezo wa kutumia vyombo vya muziki ila kuna dalili Barnaba asiweze kufikia kama walipofikia wengine.

Diamond amejitangaza zaidi yake. Mbali na kuwa huenda anazidiwa mengi ila mwenzake anaona thamani ya kipaji chake mara nyingi ziadi yake.  

Kuna kitu hakiko sawa kwa kijana. Huenda  ni usimamizi, huenda kaamua kukubali kuwa kafika au anaona muda bado. Sioni ni kwanini Barbana ashindwe kuteka soko na kuwa kule anapotamani kuwa.

Ni kwanini awe amesimama palepale toka enzi zile. Kila mmoja anampa sifa ila unaona anavyozidiwa na Ben Pol. Kila mmoja anaona ni msanii anayeweza kuwa mkubwa zaidi ila baada ya Diamond watu wanamuweka Ommy Dimpozi. Kuna nini?

Kuna sehemu inamkamata na kushindwa kumfanya kuwa mkubwa anavyostahili? Barnaba hastahili kuwa pale. Anatakwa kuwa juu zaidi ya huyo unayemwamini.  

Kuna mahali aliwahi kutajwa kama mwanamuziki na kupewa sifa kubwa sana. Ndiyo anastahili ila ni kwa namna gani ukubali sifa na kubaki palepale? Wewe ni mkali hakuna anayepinga, ila unatakiwa kuwa zaidi ya hapo.

Uangalie tena usimamizi wako. Jaribu kuchunguza kama uliposimama unastahili. Sitaki tuseme bahati. Kuna kitu cha kuchunguza kwa kina Ommy Dimpoz na Diamond. Kuna kitu wanacho, Barnaba na kipaji chake anakikosa.

Na ukali wake, kipaji chake ila mbele ya Diamond, nyuma kuna wasanii kadhaa kabla yake. Inuka ufanye kitu kijana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles