31.3 C
Dar es Salaam
Friday, December 2, 2022

Contact us: [email protected]

ALICIA, CHRISTOPHER JARECKI WAACHANA

NEW YORK, MAREKANI


KWA mujibu wa mtandao wa E! News, staa wa filamu nchini Marekani, Alicia Silverstone na baba wa mtoto wake, Christopher Jarecki, wawili hao wameachana.

Wapenzi hao wamekuwa kwenye ndoa kwa kipindi cha miaka 20, lakini miezi mitatu iliyopita kulikuwa na taarifa kwamba wapo kwenye mgogoro, hivyo mwishoni mwa wiki iliyopita wamepeana talaka.

“Bado kila mmoja atakuwa na mapenzi na mwenzake na kuheshimiana, tutabaki kuwa marafiki baada ya kuachana, tulikuwa kwenye ndoa kwa kipindi cha miaka 20, lakini kwa sasa kila mmoja na mambo yake,” alisema Alicia.

Hata hivyo, mrembo huyo ameweka wazi kuwa wataendelea kuwa kama wazazi kwa kuwa walifanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume ambaye anajulikana kwa jina la Bear Blue Jarecki, mwenye umri wa miaka sita.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,507FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles