ALI KIBA TUMEKUELEWA, SASA DONDOSHA DUDE

0
817

Na CHRISTOPHER MSEKENA

MOJA ya matukio yaliyozua gumzo wiki hii ni lile la staa wa Bongo Fleva, Ali Kiba kutangazwa kuwa mmoja ya wamiliki wa kampuni ya Rockstar4000 Music Entertainment Co &Rockstar Television ambayo amefanya nayo kazi kwa muda wa miaka 6 sasa.

Ali Kiba sasa ni mkurugenzi wa muziki na vipaji kwenye kampuni hiyo inayojishughulisha na utengenezaji wa vipindi vya mastaa mbalimbali duniani na kuvisambaza kwenye runinga za kimataifa.

Kampuni hiyo hapa Bongo inawasimimia kazi za wasanii kama Baraka Da Prince, Lady Jay Dee chini ya meneja Seven Mosha ambapo juzi, Rockstar4000 waligonga tena vichwa vya habari za burudani kwa kumtambulisha msanii Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ kuwa msanii mpya wa lebo hiyo yenye makao makuu yake Afrika Kusini.

Ommy Dimpoz ametia saini mikataba na lebo hiyokuwa msanii wa nne kusainiwa na lebo hiyo kwa mkataba wa miaka mitatu utakaokuwa unafanyiwa tathimini kila baada ya mwaka mmoja lengo likiwa ni kusimamia kazi zake za muziki.

Hizo ni habari njema kwenye tasnia ya muziki nchini, ni mwendelezo wa mapinduzi ya biashara ya muziki ambako ndiko dunia ilipo na sisi kwa harakati kama hizi tunazidi kusonga mbele.

Taarifa hizo njema haziondoi ukweli kuwa Ali Kiba ana deni kwa mashabiki zake, anadaiwa wimbo kwani ni muda mrefu umepita na kiu imekuwa kali mno ikitakiwa kutulizwa na ngoma kali kutoka kwake.

Mwaka mmoja uliopita alidongosha ngoma yake ya Aje na miezi sita baadaye akaachia toleo mbadala (remix) ya wimbo wa Aje akiwa amemshirikisha rapa kutoka Nigeria, Jude Abaga ‘M.I’.

Kutokuwepo kwa rapa huyo katika video ya Aje Remix ilipunguza mzuka wa mashabiki ambao wengi walitarajia kumuona hasa ukizingatia ilikuwa ni ngoma kali.

Sasa kimya kimekuwa kingi, Ali Kiba amekuwa mwingi wa safari, utaoina toka alipoanza ziara yake ya kuizunguka dunia ameshindwa kuachia kazi mpya.

Mwezi Januari hadi Aprili mwaka huu alifanya maonyesho kwenye nchi ya Afrika Kusini na Marekani na mwezi Juni na Julai ana maonyesho bara la Ulaya katika nchi za Ufaransa, Ujerumani Switzerland, Sweden, Uholanzi na weekendi hii atatumbuiza Ubelgiji.

Majukumu hayo yamekuwa mwiba kwa mashabiki wa Tanzania licha ya kuwaburudisha mashabiki katika nchi anazozitembelea, wengi wanahitaji kazi mpya ambayo itafanya mashabiki wake wa Bongo watambe kwa kuwa wasanii wengine wanaachia ngoma juu ya ngoma.

Inawezekana pia ukimya wa Ali Kiba unafanana kabisa na ule wa Davido mwaka jana. Msanii huyo wa Nigeria amewai kuinyooshea kidole kampuni ya Sony Music Entertainment-Africa kwa kumdumaza kimuziki.

Jarida la Pulse la Nigeria liliwahi kumnukuu Davido akiilalamikia kampuni ya Sony Music Entertainment-Africa, ilifanya asizindua wimbo wake unaoitwa How Long, kutokana na foleni ya wasanii wengi wanaotaka kuzindua kazi zao chini ya lebo hiyo ambayo Ali Kiba aliingia mkataba nao mwaka uliopita.

Sauti ya Ali Kiba ilisikika katika kolabo mbili tofauti  ambapo miezi tisa iliyopita alikikika kwenye kolanbo yake na Baraka Da Prince inayoitwa Nisamehe na akasikika pia katika kolabo yake na Ommy Dimpoz, Kajiandae.

Kazi hizo zilikuwa kubwa na kufanya Ali Kiba aendelee kutajwa kwenye chati mbalimbali za muziki lakini Baraka Da Prince alipoachia Acha Niende kukawa na Ommy Dimpoz kuwa bize kwenye safari zake nje ya nchi mashabiki wa damu  Ali Kiba wanahitaji kumsikia kwenye wimbo wake na siyo kolabo tena.

Ni kawaida ya Ali Kiba kupotea na kurudi kwa kishindo, nadhani unaikumbuka ile mwaka 2014 alipoachia Mwana, wimbo uliomrudisha kwa kishondo baada ya kimya cha miaka mitatu, hivyo basi siwezi kushangaa akiibuka na ngoma mpya muda wowote kutoka sasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here