25.6 C
Dar es Salaam
Friday, December 2, 2022

Contact us: [email protected]

ALI KIBA KUIDONDOSHA SEDUCE ME ARUSHA

MFALME wa Bongo Fleva, Ali Kiba leo anatarajia kutumbuiza ngoma yake mpya, Seduce Me kwa mara ya kwanza jijini Arusha katika tamasha la Fiesta litakalofanyika kwenye viwanja vya Sheikh Amri Abeid.

Staa huyo ambaye toka ameachia, Seduce Me iliyovunja rekodi kadhaa kwenye tasnia ya muziki Afrika, hajatumbuiza popote pale anakwenda kuonyesha ufalme wake kwa kugonga ngoma zake zote kali kwenye jukwaa la Fiesta.

Mbali na Ali Kiba wasanii wengine wa Bongo Fleva watakaokonga nyoyo za mashabiki wa Arusha ni, Rostam (Roma na Stamina), Jux, Vanessa Mdee, Lulu Diva, Rich Mavoko, Harmonize, Foby, Mua Sama, Dogo Janja, Nandy, Weusi, Chin Beez, Country Boy, Dogo Aslay, Darsaa, Bill Nas, Feza Kessy , Msaga Sumu na Ben Pol.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,504FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles