Ali Kiba, Baraka Da Prince wavamiwa Afrika Kusini

0
1026
Ali Kiba
Ali Kiba
Ali Kiba

NA BEATRICE KAIZA,

LICHA ya kuvamiwa na majambazi waliokuwa na silaha wakiwa nchini Afrika Kusini na kuporwa mali zao mbalimbali wasanii wawili wa muziki wa Bongo Fleva, Ali Kiba na Baraka Da Prince ambao wote wako chini ya lebo ya Rockstar 4000, wamesema hawatakatiza shughuli zilizowapeleka nchini humo hadi siku saba wanazotakiwa kuwepo nchini humo zikamilike.

Meneja wa Ali Kiba, Seven Mosha, alisema tukio hilo lilitokea juzi usiku saa tatu wakati wasanii hao walipokuwa katika kikao cha maandalizi ya kazi zilizowapeleka nchini humo watakapokuwepo kwa siku saba.

“Kilichotokea ndiyo hivyo siwezi tena kurudia kila wakati, taarifa ni kweli wasanii hao walivamiwa na majambazi sita waliokuwa na silaha za moto waliwapora vitu mbalimbali vikiwemo simu zao za mkononi,” alisema Seven.

Hata hivyo, Seven alisema wasanii hao wapo salama na wataendelea na shughuli zilizowapeleka nchini humo licha ya kupumzika kwa siku kadhaa kabla ya kuendelea na shughuli zao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here