Alhad aitaka serikali kuingilia kati katazo la NEMC adhana, kengele kupigwa dakika mbili

0
953

Na Christina Gauluhanga, Dar es Salaam

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum ameiomba Serikali iingilie kati kauli iliyotolewa na Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC), hivi karibuni ya kutaka kengele na adhana katika nyumba za ibada zisizidi dakika mbili kwa kuwa zinachangia uchafuzi wa mazingira kwa kelele.

Akizungumza leo Julai 9, katika Kongamano la siku maalum ya amani katika Maonyesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam, Sheikh Salum amesema ujumbe huo ni wa utovu wa nidhamu na unaweza kuchafua amani iliyopo nchini.

Sheikh Salum ambaye pia ni Mwenyekiti wa Amani mkoa wa Dar es Salaam, amesema kama sheria hiyo kweli ipo basi ibadilishwe kwakuwa inaweza kuchangia watu kukosa uhuru wa kuabudu.

“Kengele au adhana ikilia hata zaidi ya saa kumi si kelele ni moja ya kuabudu Mungu na hili lilikuwapo tangu enzi hizo,” amesema Salum.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here