31.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, January 8, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Algeria wamkataa Karim Benzema

ALGIERS, ALGERIA

KOCHA wa timu ya taifa Algeria, Djamel Belmadi, amesema wachezaji alionao wa timu hiyo wanatosha, hivyo hana mpango wa kumpa nafasi nyota wa timu ya taifa ya Ufaransa, Karim Benzema.

Benzema ambaye alikuwa mchezaji wa timu ya taifa Ufaransa, ameachwa kwenye kikosi hicho tangu mwaka 2015 kutokana na kashfa ya kumiliki mkanda wa ngono wa mchezaji mwenzake, hivyo shirikisho la soka nchini humo likaamua kuachana na mchezaji huyo kutokana na tukio hilo.

Mwishoni mwa wiki iliopita mchezaji huyo alitumia ukurasa wake wa Twitter kumuomba rais wa shirikisho hilo kumruhusu atafute taifa lingine kwa ajili ya kulitumikia kwenye soka kwa kuwa wao hawana mpango naye.

Hata hivyo zoezi hilo linaweza kuwa gumu kwa kuwa tayari aliitumikia Ufaransa kwenye michuano mbalimbali mikubwa ya kimataifa, hivyo shirikisho la soka la kimataifa FIFA linaweza lisimruhusu.

Benzema ni mchezaji mwenye asili ya nchini Algeria, hivyo ombi lake lilikuwa linaonesha wazi kuwa akikubaliwa atakwenda kuomba kujiunga na taifa hilo, lakini kocha wa timu ya taifa ya Algeria, Djamel Belmadi, amedai hana mpango wa kuwa na mchezaji huyo kwenye kikosi chake.

“Tayari kwenye kikosi changu nina Baghdad Bounedjah, Islam Slimani, Andy Delort na Hillal Soudani. Nina furaha na wachezaji hao, hivyo sina mpango wa kumuongeza mchezaji mwingine,” alisema kocha huyo.

Kocha huyo anaamini bado kikosi chake ni bora kwa kuwa kilifanikiwa msimu huu kutwaa Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Misri, hivyo Benzema hana nafasi.

Benzema mwenye umri wa miaka 31, kwa sasa yupo kwenye ubora wake wa kupachika mabao hasa akiwa na klabu yake ya Real Madrid, lakini mbali na kuwa kwenye kiwango kizuri Ufaransa hawana mpango huo wa kumuita kikosini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles